Na. Dennis Gondwe, DODOMA
SERIKALI kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 500 kutoka kwenye utaratibu wa sasa wa gharama za matumizi ya magari na kuzipeleka kwenye ununuzi wa dawa muhimu na kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya kati na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba alipokuwa akiwasilisha mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/2023 bungeni jijini Dodoma.
Dkt. Nchemba alisema kuwa serikali itatekeleza mkakati wa kubana matumizi. “Kwa upande wa hatua za muda wa kati na muda mrefu, napendekeza serikali kubadili kabisa utaratibu uliopo kwa kuwakopesha magari watumishi wenye hadhi ya kuwa na gari la serikali wawe na magari yao wenyewe, wafanye matengenezo wenyewe, wanunue vipuri wenyewe na masuala ya Mafuta yaangaliwe kwa utaratibu utakaoonekana unafaa”.
“Tutaondoa utaratibu uliozoeleka, derava na gari anapitishwa chini, bosi anapanda ndege mpaka Mwanza au Mbeya kutoka Dar es Salaam na kurudi hivyo hivyo. Kuna utafiti wa siri ulifanywa, kwa siku moja yalibainika magari ya serikali yaliyotoka Dodoma kwenda Dar es Salaam yalikuwa 132, na yaliyokuwa yanatoka Dar es Salaam yakipishana kuja Dodoma yalikuwa 76, na mengine 8 yalikuwa yamepinduka. Je, kwa mwezi ni gharama kiasi gani?”
Alisema kuwa kwa utaratibu huo, gharama za matumizi ya magari serikalini zitakuwa takribani shilingi 50,508,038,843.09. Zaidi ya shilingi bilioni 500 zitatolewa na kuelekezwa kwenye ununuzi wa dawa muhimu hospitalini, kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya kati na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Serikali ina magari zaidi ya 15,742, pikipiki 14,047 na mitambo 373 na inatumia zaidi ya shilingi 558,453,134,226.05 kwa mwaka kwa ajili ya ununuzi wa magari, ununuzi wa mafuta ya uendeshaji, ununuzi wa vipuri na matengenezo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.