NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa David Silinde amesema Serikali imeweka mkakati wa kuzipandisha hadhi barabara za udogo kwenda changarawe, changarawe kuwa lami na kuongeza fedha kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa barabara.
Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kyela Ally Anyigulile Jumbe aliyetaka kujua Je Serikali ina mkakati gani kunusuru barabara ambazo zipo katika hali mbaya sana Wilayani Kyela kwa kuwa bajeti ya TARURA haitoshi na inaletwa ikiwa na maelekezo maalum.
Silinde amesema bajeti ya TARURA Kyela kwa mwaka 2020/21 ni shilingi milioni 611,136,079.47 mwaka 2021/22 2,436,996,341.18 na mwisho kuendelea kutoa fedha za dharula kunusuru barabara zilizoathiriwa na mvua.
Aidha, amesema fedha zinazopelekwa kwa maelekezo maalum ni kwa ajili ya kutatua changamoto za muda mfupi za barababara zilizoathiriwa na mvua ili ziweze kupitika kwa wakati huo.
Ameendelea kusema kuwa Serikali iatendelea kupeleka fedha kwa ajili ya barabara kwa kuwa kwa sasa bajeti imeongezwa na tafiti zimeshafanyika kwa maeneo yenye mvua nyingi, hivyo serikali itakuja na majibu ya kunusuru barabara hizo ili ziweze kupitika wakati wote.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.