Mwenyekiti wa GPE Duniani, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada na hatua kubwa iliyofikiwa katika elimu kwa kuwezesha watoto wengi kuendelea na masomo kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari na kuongeza ufaulu kwenye ngazi zote za sekondari pamoja na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu.
Mhe. Kikwete aliyasema hayo Kibasila sekondari Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kumkaribisha Mwanzilishi wa Mfuko wa Malala ambaye (Malala Fund) aliyekuja kwa mwaliko wa Kiongozi huyo. Amesema Mfuko wa Elimu Duniani GPE umewezesha kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji wa wanafunzi na walimu kwa kujenga miundombinu ya madarasa 2980, vituo vya walimu (TRC) 252, uchapaji wa vitabu 36,118,000 matundu ya vyoo 7673, nyumba za walimu 64 na shule mpya 18 ambazo zimechangia kuleta mabadiliko nchini.
Bi. Malala Yousafzai, Mwanzilishi wa Mfuko wa Malala (Malala Fund), alisherehekea siku yake ya kuzaliwa tarehe 12 Julai, 2025, Wilayani Kongwa, Tanzania. Alieleza kufurahishwa na mazingira mazuri yanayoandaliwa kuwawezesha watoto wa Kitanzania kupata elimu. Malala alitoa wito kwa jamii na wadau kuungana kuwasaidia wasichana kutoka katika mazingira na historia tofauti ili wafikie ndoto zao. Alisema zaidi ya wasichana milioni mbili nchini Tanzania wanakosa fursa ya kuendelea na masomo, huku theluthi moja yao wakikatishwa masomo yao na kuolewa mapema. Malala alisisitiza kuwa jambo hili ni hasara kwa Taifa kiuchumi, na kuwa Serikali ikishirikiana na jamii wana uwezo wa kuhakikisha wasichana wote wanahitimu elimu yao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.