NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Festo Dugange amesema Serikali imeanza kufanya ukarabati wa shule chakavu nchini ikiwemo zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ambapo katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imetoa Sh Milioni 796 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Msingi Mshangai na Kwemsha katika Jimbo la Lushoto.
Dkt Dugange ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Lushoto, Shaban Shekilindi aliyetaka kujua ni lini serikali itakarabati shule chakavu za msingi katika Jimbo hilo.
“Katika mwaka wa fedha 2023/24 Serikali imetoa Sh Milioni 180 kwa ajili ya ukarabati wa shule kongww nne za Nyankei, Mhelo, Hemtoye na Mbaramo,” Amesema Dkt. Dugange.
Aidha, Dkt Dugange akijibu swali la Mbunge wa Mbarali, Bahati Ndingo aliyehoji ni lini serikali itakarabati shule kongwe za msingi zilizopo Mbarali amesema,
“Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa mapya na ukarabati wa madarasa chakavu. Katika mwaka wa fedha 2022/23 na 2023/24 serikali imetumia Sh Milioni 360 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa 18 mapya katika shile kongwe za Chimala, Igalako, Ujewa na Isitu.
Aidha katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali imetenga Sh Milioni 180 kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe za Ipwani, Ibumila, Mbuyuni. Lakini pia itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe kote nchini,” Amesema Dkt. Dugange.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.