MKURUGENZI wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku amesema Serikali inaendelea kuhakikisha Ulinzi na usalama wa Mtoto unazingatiwa ili kutokomeza ukatili wa aina zote kwa Watoto.
Kitiku ameyasema hayo akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Maria De Matias Wakati wa uanzishaji wa Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto ndani na nje ya Shule Mkoani Dodoma.
"Uanzishwaji wa Dawati hili Shuleni hapa utasaidia kukabiliana na Ukatili unaojitokeza ndani na nje ya shule kwenu ninyi na hata kwa watoto waliopo nyumbani na mitaani kwenu na nataka mfahamu kwamba kuna ukatili wa aina tatu kwa watoto ambao wa kwanza ni ukatili wa Kudhuru mwili, Wa pili ni ukatili wa Kingono na Wa tatu ukiwa ni ukatili wa Kihisia". alisema Kitiku.
Kitiku aliendelea kwa kusema kwamba, Serikali inazidi kupambana na wimbi la ukatili linalo sababisha watoto wengi kukatisha ndoto zao, hivyo kuwasihi wanafunzi hao kuhakikisha wanapinga vikali ukatili wakianza na kutokufanyiana ukatili wao kwa wao.
"Kumekua na wimbi kubwa la Ushoga na usagaji ambalo chanzo chake kimebainika kuwa ni ukatili wa kingono wanaofanyiwa Watoto na kusababisha kuwapotezea dira kwenye Maisha yao" alifafanua Kitiku.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu,Anna Mhina aliwaelekeza watoto vigezo vya kuzingatia kabla ya kuchagua viongozi wa madawati hayo ikiwemo kigezo cha Uadilifu.
"Mtu mwenye Uadilifu ni mtu ambaye anaweza kutunza siri utapo mwambia shida yako, Mtu anaefanya vizuri katika masomo yake ambae anaweza kubeba jukumu la ziada, Hivyo mnatakiwa kuhakikisha mnachagua viongozi watakao wasaidizi," Alisema Mhina.
Madawati ya ulinzi na usalama wa watoto 1,363 na Mabaraza ya watoto 562 katika mikoa 8 yameanziahwa tangu kampeni hii kuzinduliwa mwezi Juni, 2022.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.