Na WAF - Dar es salaam
WIZARA ya Afya na Shirika la Reli la Taifa (TRC) imeendelea kujizatiti kwa kuimarisha utayari dhidi ya ugonjwa wa Mpox, ikiwa ni muendelezo wa juhudi za Serikali kuimarisha utayari dhidi ya tishio la Ugonjwa wa Mpox hapa nchini.
Hayo yamebainishwa Desemba, 11, 2024 na Mratibu wa huduma za afya mipakani Dkt. Amour Seleman akiwa na timu ya wataalam wa afya walipotembelea kituo cha Treni ya Mwendokasi ya Magufuli jijini Dar es Salaam kuona kazi za utayari kwenye kituo hicho.
"Tukiwa kituo cha Magufuli Dar es Salaam pamoja na mambo mengine tumetathmini maeneo kwa ajili ya kuweka Televisheni za kutolea elimu kwa wasafiri, huduma za ukaguzi kiafya, sehemu za kuweka vipimia joto (Mass Walkthrough Thermoscanner) pamoja na ofisi kwa ajili ya watumishi wapya waliopangiwa kufanya kazi vituo vya SGR," amesema Dkt. Amour.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa TRC, Dkt. Peter Mganya ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Afya kwa kipindi chote cha maandalizi ya utayari wa kukabiliana na tishio la Mpox hapa nchini ili kuwahakikishia usalama wa kiafya wateja wote wanaotumia huduma za TR
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.