MKURUGENZI wa Idara ya TEHAMA Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI), Erick Kitali amewashukuru wadau
wa maendeleo KOICA na PMC kwa kuendelea
kushirikiana na Serikali katika kuimarisha
usimamizi wa taarifa za utoaji wa huduma za afya
kupitia mfumo wa usimamizi wa taarifa za vituo
vya afya (GoT-HOMIS) katika Mkoa wa Dodoma.
Kitali amebainisha hayo katika kikao kazi cha Kamati ya Ushauri ya mradi wa upanuzi wa matumizi ya mfumo wa GOT-HOMIS katika Mkoa wa Dodoma.
"Tuendelee kushirikiana kwa pamoja kutimiza
malengo ya mradi na kuleta ufanisi katika utoaji wa
huduma za afya kwa wananchi" Ameeleza Kitali
Lengo la kikao hiko ni kupitia na kujadili utekelezaji
wa mradi huo pamoja na kuweka mipango madhubuti ya utekelezaji wa mradi ili kuongeza wigo na kuboresha matumizi ya mfumo wa GOT-HOMIS katika vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Dodoma.
Mfumo wa GoT-HOMIS ambao kwa sasa unatumika
kwenye vituo zaidi ya 1,400 nchi nzima, umelenga
kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika vituo
vya kutolea huduma za afya, kutoa taarifa za
magonjwa na wagonjwa kwa usahihi na wakati na
kusimamia rasilimali fedha na dawa.
Kikao kazi hicho kimehusisha wataalam kutoka
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI), Wizara ya Afya, Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, wadau wa maendeleo KOICA
pamoja na PMC.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.