• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yajipanga kuimarisha sekta ya Uvuvi nchini

Imewekwa tarehe: November 27th, 2020

SERIKALI kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ipo katika mchakato wa kukamilisha  Mpango Kabambe wa miaka 15 ijayo kuanzia 2021 utakaosimamia sekta ya Uvuvi na kutoa dira ya kulinda rasilimali za uvuvi ili sekta hiyo iweze kutoa mchango mkubwa na endelevu katika pato la taifa.

Hilo limefahamika wakati Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (pichani juu akifungua Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi wa kupitia, kujadili na kuidhinisha masuala ya kipaumbele yanayopaswa kuingizwa katika Mpango huo Kabambe unaofanyika Mkoani Singida kuanzia Novemba 26-28, 2020.

Dkt. Tamatamah alisema kuwa lengo la Serikali ni kuona sekta ya Uvuvi inaendelea kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa zaidi ya ilivyosasa na ndio maana inaandaa mpango huo ili usimamizi wa rasilimali za uvuvi uwe imara.

“Ni mategemeo yetu kuwa mpango huu utatoa hamasa kwa sekta ya uvuvi katika kulinda usalama wa chakula kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa, vilevile tunatarajia utuingize katika uchumi wa viwanda na uchumi wa bluu,” alisema Dkt. Tamatamah.

Alisema kuwa pamoja na juhudi za Wizara za kusimamia maendeleo ya Sekta ya Uvuvi nchini, Sekta hiyo imeendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kwa ujumla zimekuwa zikiathiri ukuaji na uendelevu wa sekta hiyo.

Aliendelea kueleza kuwa ili kukabiliana na changamoto hizo, Wizara imekuwa ikitekeleza mipango, mikakati na programu mbalimbali zinazolenga kuendeleza sekta ya uvuvi nchini, miongoni mwa mipango hiyo ni Mpango huo Kabambe wa Uvuvi unaotarajiwa kuanza kutumika mwaka 2021.

Mratibu wa Masuala ya Uvuvi kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), ambao wanafadhili maandalizi ya mpango huo, Dkt. Oliver Mkumbo alisema shirika hilo limeamua kufadhili mpango huo ikiwa ni sehemu ya malengo yao ya kuhakikisha dunia inaondokana na njaa, umasikini na kuimarisha usalama wa chakula ili ifikapo mwaka 2030 pasiwepo na mtu atakayekuwa na njaa.

Aidha, wadau wa Sekta ya Uvuvi hawakusita kuonesha matumaini yao na mpango huo huku wakisema kuwa ukikamilika utajibu changamoto nyingi ambazo zimeendelea kuikabili sekta hiyo.

Kiongozi wa Wavuvi Mkoani Kigoma, Francis John alisema kuwa mpango huo ambao utasimamia rasilimali za uvuvi utawasaidia kuimarisha biashara yao ya dagaa kutoka ziwa Tanganyika kwani mpango huo utawahakikishia uwepo wa dagaa wengi ambapo wataweza kuwa na mzigo wa uhakika wa kusafirisha kwenda kuuza dagaa wao katika nchi za Marekani, Astralia, Kanada, Uingereza na Denmark.

Naye, Raphael John, mdau wa sekta hiyo ya Uvuvi alisema kuwa  moja ya mambo yatayokwenda kuimarishwa kupitia mpango huo ni ufugaji na ukuzaji wa viumbe maji jambo ambalo anasema litasaidia kupunguza utegemezi wa kupata mazao ya uvuvi kutoka maji ya asili pekee.

“Katika nchi nyingi zilizoendelea, ufugaji na ukuzaji wa viumbe maji umepewa kipaumbele sana, ni muhimu kuimarisha eneo hilo ili tusitegemee tu uvuvi wa mazao ya samaki katika maji ya asili, ni lazima tuanze sasa kabla rasilimali za asili katika bahari, mito na maziwa hazijaisha,” alisema John

Mpaka sasa sekta ya uvuvi inachangia asilimia 1.7 katika pato la Taifa huku ikielezwa kuwa sekta hiyo inatoa ajira ya moja kwa moja kwa wananchi takriban 202,000 na wananchi wengine wasiopungua Milioni 4.5 wanaendelea kutegemea kupata kipato chao kupitia sekta hiyo.

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) limetoa Dola za Kimarekani 195,000 kwa ajili ya kufanya mapitio na kuandaa Mpango Kabambe huo wa sekta ya uvuvi ili sekta hiyo iweze kusimamiwa vizuri na kuendelea kuleta maendeleo yenye tija nchini.

Uandaaji wa mpango huo ni sehemu ya mipango mingi ambayo serikali imekusudia kuitekeleza, wakati akifungua Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 13, 2020 jijini Dodoma, Mhe. Rais, Dkt. John Joseph Magufuli alieleza mipango kadhaa ya kuboresha sekta ya uvuvi ikiwemo ununuzi wa meli nane (8), ujenzi wa Bandari kubwa ya uvuvi itakayotoa ajira elfu thelathini (30,000).


Sehemu ya Wadau wa Sekta ya Uvuvi wakiwa makini kufuatilia matukio katika Mkutano wa kupitia, kujadili na kuidhinisha masuala ya kipaumbele ya Mpango Kabambe unaofanyika Mkoani Singida Novemba 26-28, 2020.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Sekta ya Uvuvi walioshiriki Mkutano wa kupitia, kujadili na kuidhinisha masuala ya kipaumbele ya Mpango Kabambe unaofanyika Mkoani Singida Novemba 26-28, 2020.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.