KATIKA kuhakikisha kila mtoto anapata Elimu bora bila kujali hali aliyonayo, serikali imenunua vifaa wezeshi vyenye thamani ya zaidi ya Tsh.Bilioni 2.8 vitakavyonufaisha wanafunzi wenye mahitaji Maalum 18,488 kote nchini.
Akizungumza leo Januari 14, 2021 katika zoezi la uzinduzi wa vifaa hivyo wezeshi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, zoezi ambalo limefanyika Shule ya Sekoandari Dodoma,Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo amesema jumla ya vifaa Wezeshi 51,339 vimetolewa kwa watoto wenye mahitaji maalum 18,488 lengo ni kuhakikisha kila motto anapata elimu bora.
Aidha,Waziri Jafo amefafanua kuwa zaidi ya Tsh.Trioni 1.03 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya elimu bila malipo hadi kufikia Mwishoni Mwa Mwaka jana.
Hata hivyo ,Waziri Jafo amesisitiza utunzaji wa vifaa vipya vilivyotolewa ili viweze kusaidia wenye uhitaji kwa muda mrefu.
Kwa upande Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanaga amesema vifaa hivyo vinalenga kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wakiwemo Wenye ulemavu wa akili,ulemavu wa viungo ,wasioona,viziwi,uoni hafifu ,ulemavu wa ngozi huku akibainisha kuwa shule zinazohudumia wenye mahitaji maalum zimeongezeka kwa asilimia 46.1 % ikiwa elimu ya Msingi 23.9% ,sekondari ni asilimia 24.6% .
Aidha,Mhandisi Nyamhanga amebainisha idadi ya wanafunzi wenye ulemavu waliohitimu elimu ya msingi na kujiunga na elimu ya Sekondari imeongezeka kutoka asilimia 69.9% (wanafunzi 1117) kwa mwaka 2016 hadi asilimia 76.3% (Wanafunzi 2534) kwa mwaka 2020 huku bilioni 42.3 zimetumika kama chakula kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika kipindi cha miaka mitano.
Mkurugenzi anayeshughulikia Elimu Maalum Ofisi ya Rais ,TAMISEMI Julius Migeha amesema serikali inaendesha zoezi la kubaini Watoto wenye mahitaji maalum katika kata zote 3956 kote nchini ambapo ametoa wito kwa wazazi kutoa ushirikiano huku Mwanafunzi mwenye Mahitaji Maalum Jackline Lazaro akitoa shukrani kwa kupata msaada huo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.