WAJANE nchini wameiomba Serikali kuwapa kuandaa sera ya Taifa itakayowatambua kama kundi maalum katika jamii ili haki zao ziweze kulindwa.
Wametoa kauli hiyo imetolewa wakati wa maandamano yaliyohitimisha maadhimisho ya siku ya wajane duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Nyerere Jijini Dodoma leo.
Mmoja wa Wajane hao Nyabumera alisema “tunaiomba Serikali itoe ushirikiano na kusaidia uanzishaji wa Sera ya taifa ya wajane itakayowatambua wajane kama kundi maalum katika jamii” alisema.
Alisema uanzishwa kwa sera ya Taifa kwa ajili ya wajane kutasaidia kutoa msukumo kwa jamii juu ya haki na madhila wanayopitia wajane na kwamba kundi hilo limekuwa likidhulumiwa mali pindi wenzi wao wanapofariki.
Nyabumera alishauri vifo vya wanaume vitambuliwe kuwa vinatokana na mapenzi ya Mungu kama vilivyo vifo vya wanawake. “Pendekezo langu vifo vya wanaume navyo vitambuliwe kuwa vinatokana na mapenzi ya Mungu kama vilivyo vifo vya wanawake na siyo kurogwa, jambo hilo ndilo linalosababisha wajane tunakosa haki zetu baada ya kufiwa na waume zetu” alisema Nyabumera huku akishauri jamii ijenge utamaduni wa kuandika wosia ili kuwasaidia wenzi wao kuwa salama na kumiliki mali walizochuma pamoja na waume zao.
Nae mkazi wa Jijini Dodoma, Lusy Sanga alisema kuwa wajane wamekuwa wakipitia mateso makubwa na kuangukia katika wimbi la umasikini. “Baada ya mume wangu kufariki, ndugu wa mume walichukua mali zote na kuuza nyumba” alisema Sanga na kufafanua kuwa baada ya tukio hilo hali ya maisha ilibadilika na kuwa ngumu jambo lililomlazimisha kufanya kazi usiku na mchana ili kuweza kuwahudumia watoto wake saba.
Akiongelea changamoto zinazowakabili wanawake wajane, mkazi wa Mwanza Antonia Zacharia aliyeshiriki maadhimisho hayo alisema kuwa, wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazodidimiza juhudi zao za kujiletea maendeleo.
Alisema miongoni mwa changamoto hizo ni kutengwa na ndugu wa mume baada ya mume kufariki na wajane kunyanyaswa na kunyang’anywa mali zote na ndugu wa mume wakidai kuwa ni mali zao na pale wanapolazimika kudai mali hizo hutakiwa kutoa rushwa na ngono.
Maadhimisho ya siku ya wajane duniani yamefanyika kitaifa jijini Dodoma yakiwa ni maadhimisho ya kwanza kufanyika kitaifa yakiongozwa na kaulimbiu isemayo “Wezesha mafunzo ya ujuzi kwa wajane: Changia kufikia malengo ya maendeleo endelevu”, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustine Dugulile.
Maandamano ya wajane wakielekea uwanja wa Nyerere Square kuhitimisha Siku ya Wajane Duniani.
Wajane wakiandamana kitaifa kusherehekea siku ya wajane duniani
Wanawake wajane wakipaza sauti kukemea changamoto wanazokutana nazo kwenye maisha ya ujane
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.