Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI
MWENYEKITI wa maafisa lishe wa mikoa na halmashauri, Benson Sanga ameiomba serikali kuajiri maafisa lishe ngazi ya kata, kijiji na mtaa ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za lishe nchini
Akizungumza kwa niaba ya maafisa lishe leo Julai 16, 2024 jijini Dodoma kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Maafisa Lishe wa Mkoa na Halmashauri nchini amesema upungufu wa maafisa lishe kwenye ngazi ya kata unaathiri utendaji kazi na kupunguza ufanisi katika utoaji wa huduma za lishe katika ngazi ya jamii.
Amesema kuwajiriwa kwa wataalamu hao kutasaidia kuongeza kasi ya usimamizi na utoaji wa huduma za lishe zenye ubora katika ngazi ya jamii ikiwemo utoaji wa elimu ya lishe na ushauri wa kilaamu wa lishe.
Aidha, Sanga ameiomba serikali kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya afua za lishe zinatolewa kwa wakati ili ziweze kutekeleza afua za lishe na kufikia malengo yaliyopangwa.
Pia ameshauri kuwa matumizi ya fedha za lishe yaingizwe kwenye vipaumbele katika ripori ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili matumizi yake yafuatiliwe kwa karibu.
Sanga alisema pia kumekuwa na changamoto ya ukosefu wa chakula dawa, cha kununua kutoka Bohari ya Dawa (MSD).
“Tunaiomba Serikali kuielekeza MSD kuagiza chakula dawa ili vituo viweze kununua kwa urahisi na pia tunaiomba Serikali iendeleze juhudi za kuanzisha kiwanda cha kutengeneza chakula dawa hapa nchini.”
Pia, ameiomba Serikali kuweka kanuni za kusimamia uongezaji wa virutubisho kwenye vyakula vinavyosindikwa na viwanda vya kati na vidogo na ukosefu wa vifaa na bidhaa za huduma za lishe.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.