• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yapaisha ustawi wa watu Wasioona nchini

Imewekwa tarehe: October 21st, 2022

SERIKALI ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imefanikiwa kuwawezesha Watu wasioona hususan katika eneo la Ajira, Michezo na TEHAMA.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, amebainisha kuwa serikali kupitia Mwongozo wa Viwango vya Vifaa vya TEHAMA wa mwaka 2020 umejumuisha mahitaji ya watu wasioona ili kuweka mazingira rafiki kwenye Ofisi za Umma na maeneo ya kutolea huduma kwa Wananchi.

Ameyasema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wasioona Kitaifa yaliyofanyika Babati Mjini, Mkoani Manyara tarehe 21 Oktoba, 2022 yaliyobebwa na kauli mbiu isemayo “Ujumuishwaji wa Watu Wasioona katika Ajira, Michezo na TEHAMA kwa Maendeleo Endelevu".

Amebainisha kuwa serikali imeendelea kutoa Ajira kwa Watu wenye Ulemavu wakiwemo wenye ulemavu wa kutoona ambapo kwa mwaka 2022 Ajira zilizotolewa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI za Kada ya Walimu nafasi 9,800 na Kada za Afya 7,612 jumla ya Watu wenye Ulemavu 261 sawa na 2.7% walikidhi vigezo na kupata ajira ya ualimu,

"Kati ya hao 261 Watu wasioona walikuwa 61 (Ke. 13 na Me.49). Vilevile, kwa upande wa Kada za Afya jumla ya Watu wenye Ulemavu 42 walikidhi vigezo na kupata ajira ambapo miongoni mwao wasioona walikuwa wanne (4) Ke. 1 na Me.3"

Katambi amefafanua kuwa serikali ya Mhe. Rais Samia inatambua na kutoa kipaumbele kwa masuala ya Watu wenye Ulemavu, ambapo tayari imezindua Mwongozo wa Taifa wa Utambuzi wa Mapema na Afua Stahiki kwa Watoto wenye Ulemavu. "Lengo kuu la kuzindua mwongozo huu ni kusaidia kuwatambua Watoto wenye ulemavu na kusaidia kuweka mipango mbalimbali ikiwemo ya elimu na afya ili kuwapunguzia makali ya ulemavu na pengine kuuondoa kabisa".

Aidha, Katambi ameongeza kuwa Serikali imeona ipo haja ya kuhakikisha Watoto wenye ulemavu wanapata elimu kama Watoto wengine wasio na ulemavu na hivyo kutunga Sera ya Elimu Jumuishi, hii ni hatua ya kuhakikisha kuwa Watoto wenye ulemavu wa kawaida wanaweza kupata elimu pamoja na watoto wengine katika maeneo yao.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.