SERIKALI imekuwa ikipeleka fedha moja kwa moja katika vituo vya Afya ili kupunguza urasimu unaosababisha kuchelewa kwa huduma zinazotakiwa kutolewa.
Kauli hiyo ilitolewa na mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Joseph Mdachi alipokuwa akiongea na timu ya wataalam wa Kituo cha Afya Mkonze na viongozi wa Kata ya Mkonze, kikao kilifanyika katika kituo hicho.
Dkt. Mdachi alisema kuwa serikali inaleta fedha moja kwa moja kituoni. “Kwa kuwa serikali inaleta fedha moja kwa moja kituoni, changamoto ya fedha, huduma na dawa zinatakiwa kushughulikiwa katika ngazi ya kituo na kata.
Wakati huohuo, alisisitiza kina mama wajawazito kuhamasishwa kuhudhuria kliniki pale wanapojigundua kuwa wajawazito. “Mchakato wa mama mjamzito kujifungua siyo kitendo cha dharura kwa sababu kuna muda wa miezi tisa ya ujauzito. Changamoto kubwa ni wakina mama wengi wanachelewa kuanza kliniki na baadhi yao kufariki kwa kupoteza damu” alisema Dkt. Mdachi.
Alisema kuwa mama mjamzito anapohudhuria kliniki mapema anashauriwa kitaalam kuelekea kujifungua salama. “Katika kipindi hicho, kutokana na uchunguzi wa kitaalam, mama atashauriwa kama itabidi kujifungulia katika hospitali kubwa ili familia ianze kujiandaa mapema” alisema Dkt. Mdachi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.