• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yapunguza gharama kwa wagonjwa wenye matatizo ya moyo

Imewekwa tarehe: July 11th, 2019

Asilimia tisini (90%) ya wagonjwa wanaokabiliwa na matatizo ya moyo waliokuwa wanatibiwa nje ya nchi, hivi sasa wanatibiwa ndani ya nchi kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete (JKCI).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, alipofanya ziara kwenye hospitali ya JKCI ambapo alitembelea  jengo la watoto lililofanyiwa ukarabati hivi karibuni.

Dkt. Ndugulile alisema Serikali inaendelea kufanya maboresho ya sekta ya afya kuanzia huduma za msingi hadi za kibingwa kwa kuwezesha vituo zaidi ya 352 kutoa huduma za upasuaji wa dharura wa kumtoa mtoto tumboni.

Alisema hivi sasa ujenzi wa hospitali 67 za wilaya unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba tangu Uhuru kumekuwako na hospitali 70 za Wilaya pekee, hivyo idadi itaongezeka.

“Nawapongeza sana JKCI kwa maboresho makubwa mliyofanya katika jengo ya watoto ni ya kiwango kikubwa sana, hongereni sana, hivyo hatutarajii hospitali kama hii iwe inatibu magonjwa madogo madogo ambayo yanaweza kutibiwa kwenye hospitali za rufaa za wilaya au mikoa,” alisema.

Aliongeza kusema kuwa, katika miaka minne ya uongozi, serikali imeweza kupiga hatua kubwa ikiwamo kupunguza idadi ya wagonjwa wengi waliokua wanatibiwa nje ya nchi.

“Kwa hatua hii, tumeweza kupunguza gharama za matibabu nje ya nchi, tulikuwa tunaweza kuhudumia watu wachache lakini kwa kuwa matibabu yanapatikana hapa hapa nchini, wananufaika watu wengi. Kwa gharama ile ile ambayo nje ya nchi angetibiwa mtu mmoja, hapa nchini wanatibiwa watu wapatao watatu,” alibainisha.

Alisema mafanikio hayo ni matokeo ya hatua za kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mafunzo madaktari wa ndani (wazalendo) ambapo sasa wanaweza kufanya upasuaji mkubwa wao wenyewe.

“Hivyo, Serikali itaendelea kuwapatia mafunzo wataalam wa afya na kuwapatia vibali kwenda kujifunza ama kusoma nje ya nchi ili kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini na kuweza kuwatibia wananchi.

Aidha, katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile alipokea vifaa vya kuzima moto vipatavyo kumi na mbili vya hospitali hiyo kutoka kampuni ya SUKOS Kova Foundation inayomilikiwa na Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova, kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution ya hapa nchini.

Dkt. Ndugulile alisema Watanzania wengi wanafariki wakati wa uokoaji kwani watu wengi hawana elimu ya uokoaji kwani zipo kanuni zinazotumika wakati wa  kumuokoa mtu anayepata ajali.


Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza na mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya moyo Asha Luhomo wakati wa ziara yake kutembelea taasisi hiyo.


Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza na mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake kutembelea taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

Chanzo: afyablog.moh.go.tz


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.