Serikali leo imetia saini mikataba miwili ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa Barabara ya lami ya njia nne ya Mzunguko (Outer Ring Road) ndani ya Jiji la Dodoma itakayokuwa na urefu wa kilometa 112.3 na kuwa barabara ndefu za aina hiyo kuliko zote katika Nchi za Afrika Mashariki na Kati na kutatua changamoto ya msongamano wa magari jijini Dodoma.
Mikataba iliyosainiwa ni baina ya Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa niaba ya Serikali na wakandarasi wawili Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) na AVIC INTL Project Engineering Company walioshinda zabuni ambao watajenga barabara hiyo kwa kipindi cha miezi 36. Mkandarasi Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), atajenga kilometa 52.3 kuanzia Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port na mkandarsi AVIC INTL Project Engineering Company atajenga kilometa 60 itakayoanzia Ihumwa Dry Port – Matumbulu hadi Nala.
Mradi huu utahusisha Ujenzi wa Vituo vya Afya pamoja na magari ya wagonjwa (Ambulance) matano katika maeneo ya Ihumwa, Nala, Mahomanyika na Veyula.
Aidha, itajumuisha uchimbaji wa visima virefu vya maji katika maeneno ya Ihumwa, Mahomanyika, Nala na Veyula.
Vilevile, kutakuwa na ukarabati wa Shule ya Msingi Chilwana Ihumwa na ukarabati wa barabara za Mwangaza-Medeli-Kizota-Zuzu zenye jumla ya Kilometa 28.37.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.