Mahakama ya Jumuiya Afrika Mashariki imetupilia mbali madai ya kupinga uhalali wa Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao umeundwa Aprili 26, 1964 na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar (wakati huo) na Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika (wakati huo), ambapo shauri hilo lilifunguliwa na baadhi ya wanaharakati wa Zanzibar.
Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata ameeleza kuwa mahakama hiyo imetoa uamuzi huo baada ya kukubaliana na hoja zote za upande wa Serikali ikiwa ni pamoja na madai kuletwa nje ya muda, pamoja na uhalali wa mahakama kuhoji uhalali wa muungano huo.
Amesema Mahakama ya Afrika Mashariki imezaliwa kupitia makubaliano (The East African Community Treaty) ya mwaka 1999 na kuanza kufanya kazi mwaka 2000, hivyo mahakama hiyo haina mamlaka ya kuhoji Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964.
OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU USIKILIZWAJI NA UAMUZI WA SHAURI NAMBA 09/2016 KATIKA MAHAKAMA YA HAKI YA AFRIKA MASHARIKI BAINA YA RASHID SALUM ADIY NA WENZAKE 39,999 DHIDI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, KATIBU MKUU KIONGOZI WA BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI, TAREHE 29/9/2020 SAA 3:30 ASUBUHI
1. UTANGULIZI
2. USIKILIZWAJI WA SHAURI
• Shauri lilisikilizwa tarehe tarehe 6/7/2020 kwa njia ya Video ( Video Conference) ambapo wadai waliwakilishwa na Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wa Tanzania pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar ambao ni;
• Upande wa Walalamikaji uliwakilishwa na Wakili Rashid Mutola
HOJA ZA SERIKALI KATIKA MAPINGAMIZI YA AWALI:
• Serikali ilipinga uwezo wa Mahakama kusikiliza Shauri linalohusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa hoja zifuatazo
HOJA ZA WALALAMIKAJI KUHUSU MAPINGAMIZI YA AWALI.
Walalamikaji kupitia Bw. Rashid Mutola walipinga hoja za Serikali kwa hoja kwamba Mahakama ina mamlaka na malalamiko ya wateja wake yanahusu haki za binadamu kwani wakati wa kuanzishwa Muungano wananchi wa Zanzibar hawakushirikishwa. Aidha, walalamikaji walidai kwamba madai yao ni ya msingi.
Na hivyo waliomba mapingamizi ya Serikali yatupiliwe mbali na shauri liendelee kusikilizwa kwa wahusika kuendelea kutoa ushahidi kama ilivyokubaliwa kwenye Kongamano la pamoja (scheduling conference).
UAMUZI WA MAHAKAMA:
Shauri hili limetolewa uamuzi tarehe 29/9/2020 kwa njia ya Video (Video Conference). Katika Maamuzi yake, Mahakama imekubaliana na hoja zote za Serikali kuhusu kutokuwa na uhalali wa kisheria wa Mahakama kusikiliza Shauri hilo. Pamoja na mambo mengine, Mahakama imekubaliana na hoja zote za Serikali. Katika uamuzi wake Mahakama ilieleza mambo yafuatayo:-
Mahakama haina mamlaka ya kisheria kuhoji uwepo Taifa huru wa Jamhuri ya Muungano Tanzania ikiwa ni pamoja kutoka tafsiri ya maamuzi ya nchi mbili huru zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo kwa mujibu wa Mkataba wa Uanzishaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanganyika na Zanzibar sio nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki
Mahakama imekubaliana na hoja kwamba, wadai hawana hoja yoyote dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani wadai wameshindwa kuthibitisha madai yao kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo wakati Hati za Muungano zinasajiliwa katika Umoja wa Mataifa na kutambuliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna mapingamizi yaliyowasilishwa kupinga hati za Muungano kutoka kwa Tanganyika au Zanzibar.
Mahakama pia ilikubaliana na hoja madai yaliwasilishwa nje ya siku 60 zinazotajwa katika ibara ya 30(2) ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kuhusu gharama, Mahakama imeamua kila upande ubebe gharama zake kwa kuzingatia kwamba shauri hilo liliwasilishwa kwa kuzingatia maslahi ya Umma (public interest).
Mwisho, Shauri hili limetupiliwa mbali kwa hoja zilizotajwa hapo juu.
Imeandaliwa na
Gabriel Pascal Malata,
Wakili Mkuu wa Serikali,
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali,
Dar es Salaam, 30 Septemba 2020.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.