• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yasikia kilio cha wananchi tozo miamala ya simu

Imewekwa tarehe: July 20th, 2021

WAZIRI wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema Serikali imesikia kilio na maoni ya wananchikuhusu tozo mpya ya miamala ya simu na kuwaomba wawe watulivu wakati jambo hilo linatafutiwa ufumbuzi.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari akiambatana na Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Dkt. Faustine Ndugulile.

“Kwa maaneo ambayo wananchi wametoa ushauri na kuelezea namna ambavyo jambo hili linawagusa lakini pia tumepokea maeneo ambayo yanatakiwa kutoa elimu zaidi ili kujenga uelewa wa pamoja ikiwa ni pamoja na viwango vinavyokatwa kwa anayetuma na anayetoa lakini pia kuhusu mantiki ya jambo lenyewe” alisema Mhe. Mwigulu

Alisema kuwa jambo la tozo za miamala linatekelezwa kupitia Sheria iliyopitishwa na Bunge lakini kuna Kanuni za utekelezaji zinazo mhusu yeye kama Waziri wa Fedha na Mipango na maeneo mengine yanahusu Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambazo zitajadiliwa na kupatiwa ufumbuzi.

Dkt. Nchemba alisema kuwa siku ya Jumanne tarehe 20 Julai, 2021 kutakuwa na kikao kilichoitishwa na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, kujadili suala hilo na pia kutakuwa na kikao kingine cha Mawaziri wa Wizara zote kuchambua kwa kina suala hilo.

“Lakini Tayari Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan naye alishaguswa na jambo hili, amesikia maoni ya watanzania wote na yeye ametolea maelekezo kwamba tuyafanyie kazi maoni hayo, Nitoe Rai kwa wananchi kuwa watulivu kwenye jambo hili, tutaendelea kuelezea na kutoa ufafanuzi kwenye kila maeneo yanayohitaji ufafanuzi na tutachukua hatua kwenye maeneo wanayohitaji kuchukuliwa hatua ili ujenzi wa taifa letu uendelee kama ambavyo wananchi wamekuwa na shauku kubwa kuona ujenzi wa Taifa letu unaendelea kwa ajili ya maendeleo ya nchi” Aliongeza Dkt. Nchemba

Dkt. Nchemba aliwaonya watu wenye nia mbaya ambao mara zote wanapenda kupotosha ama kubadili dhana au maana halisi ya jambo lilivyokusudiwa na kuwataka wasifanye hivyo, kwani mambo haya yana maslahi mapana kwa nchi.

“Haya ni mambo ya kisheria, Sheria za nchi zinatakiwa kuheshimiwa, ni mambo ambayo ni ya kikanuni  yanayohitaji uelimishaji. Tutaendelea kufafanua lakini yale yanayotakiwa kufanyiwa kazi niwaahidi watanzania, tutaendelea kuyafanyiakazi kama ambavyo viongozi wetu wakuu wamesema” Alisisitiza Mhe. Nchemba

Alisema tayari aliwapa maelekezo wataalam wa mifumo kuangalia vipengele vya Sheria ya Mifumo ya malipo Serikalini pamoja na Sheria ya Mawasiliano ya Mtandao (EPOCA) inayoelezea kuhusu masuala ya miamala kwa njia ya mtandao na kuja na mapendekezo yatakayosaidia kufikia muafaka wa jambo hilo.

Alitoa Rai  kwa watanzania waendelee kumuunga mkono Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika Dira yake ya kuhakikisha anasukuma mbele shughuli za maendeleo ya nchi na ili tuwakomboa na kuwakwamua wananchi kiuchumi.

Kwa upande wake Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Mheshikiwa Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) alibainisha kuwa Wizara yake pia ambayo inaguswa moja kwa moja na tozo hizo imeendelea kupokea maoni na kuchakata taarifa mbalimbali tangu tozo hiyo ianzishwe na kumwahidi Waziri wa Fedha na Mipango kwamba atampa ushirikiano kuhakikisha kwamba maelekezo yaliyotolewa na viongozi yanatekelezwa.

Alirejea kutoa wito kwa watanzania kuwa watulivu wakati jambo hilo linafanyiwa kazi na kusema kuwa Serikali ni sikivu na itafikia muafaka mzuri.


Imeandikwa na Benny Mwaipaja, Afisa Habari Wizara ya Fedha, Dar es Salaam


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.