• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yasisitiza kulinda haki za watoto wenye magonjwa adimu

Imewekwa tarehe: February 28th, 2021

SERIKALI ipo tayari kuweka mazingira sahihi na ya kisera ili kuhakikisha watoto wenye magonjwa adimu wanapata haki sawa na kutoachwa nyuma katika kuwahudumia.

Hayo yamesemwa jana na Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya Magonjwa Adimu duniani yaliyofanyika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mama Samia amesema Serikali haijawaacha nyuma watoto hao na kwamba ina nia, dhamira na sababu ya kufanya mazingira wezeshi ya kuwahudumia kwani magonjwa hayo ni kama magonjwa mengine.

Ametoa wito kwa wazazi wenye watoto hao kutowaficha na hivyo kuongeza sauti ili kuweza kuwaamsha wengine kujitokeza, hiyo itaisaidia Serikali kubaini haja iliyopo na kuweza kutoa matibabu sawa.

Awali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima ameahidi Wizara hiyo ipo tayari kupokea maoni na mawazo kutoka kwa wadau na wazazi wenye uzoefu wa kuwahudumia watoto wenye magonjwa adimu na kuyaingiza kwenye mapitio ya Sera mpya ili iwe na sura inayotambua mapambano yanayotakiwa kufanywa kwenye eneo hilo.

Dkt. Gwajima amesema wizara yake itaendelea kushirikiana na wadau pamoja kutengeneza mpango kazi wa namna wa kuongeza kasi ya kuimarisha huduma za magonjwa adimu nchini ili kuleta usawa na usawia katika makundi yanayoathirika na magonjwa hayo ili wajisikie na wenyewe ni sehemu halali kabisa ya jamii na wanayopambana nayo kwamba yanawahusu wote.

Vilevile Dkt.Gwajima amesema wizara inakamilisha mpango mkakati wa huduma shufaa na utengamao utakaoongeza kasi na ubora wa huduma hizo kwani muelekeo wa sekta ya afya ni kuyapa malengo ya kipaumbele.

Hata hivyo wizara ya afya imepitia mpango mkakati wa sekta ya afya wa kuzuia na kudhibiti Magonjwa yasiyo ambukiza ambapo magonjwa adimu yamewekewa malengo ya kipaumbele .

Naye, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi amewapa pole na kuwapongeza wazazi wote nchini wenye watoto wanaougua magonjwa adimu.

Prof.Makubi amesema Serikali imefanya juhudi kubwa kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa hao na kuweka miundombinu na utayari wa nchi upo.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.