• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yasisitiza matumizi ya Mbolea

Imewekwa tarehe: January 7th, 2023

SERIKALI imehimiza matumizi ya mbolea kwa wananchi wa Kijiji cha Mlali Iyegu kilichopo Kata ya Mlali katika Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma ili kuepuka upungufu wa chakula kwa kuzalisha mazao kwa wingi kwa kutumia mbolea inayotolewa kama ruzuku kutoka Serikalini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule alipokua akiongea na wananchi hao wakati wa ziara yake iliyolenga kusisitiza utunzaji wa mazingira, kilimo na kukahamasisha agenda ya elimu.

"Asilimia 90 ya Wakazi wa Kongwa ni wakulima na wanategemea kilimo kuendesha maisha yao. Nawasisitiza kufanya kilimo cha kisasa kwa kutumia mbolea kwani Serikali imeamua kuwapunguzia mzigo wa gharama kwa kuchangia asilimia 70 ya gharama hizo. Hakuna Serikali inayotaka kudhuru watu wake, mbolea inayotolewa ni bora na imepimwa kitaalamu. Hatutarajii kupata maombi ya chakula cha msaada kutoka Serikalini wakati uwezekano wa kutumia pembejeo bora na kupata chakula cha kutosha upo" Amesema Senyamule. 

Katika ziara hiyo pia, Senyamule aliweza kutembelea shule mpya ya Sekondari iliyojengwa kwa fedha za Serikali iliyopo katika Kijiji cha Ihanda, Kata ya Mlali inayotarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Januari 9 mwaka huu. Shule hii inatarajiwa kuwa msaada kwa wanafunzi wa Kijiji hicho ambao walikua wakitembea umbali mrefu wa takribani kilometa 12 kila siku kwenda na kurudi.

"Nimefurahishwa na ukamilishwaji wa shule hii ambayo itaepusha watoto kutembea umbali mrefu kufuata shule ya Sekondari Mlali. Serikali imetimiza wajibu wake hapa na wazazi mtimize wajibu wenu wa kuhakikisha watoto wanafika hapa shuleni" Amesisitiza Senyamule

Mkuu wa Wilaya hiyo Remidius Mwema, amesema kuwa walipokea fedha za ujenzi wa madarasa 70 katika Wilaya yake na yote yamekamilika hivyo watahakikisha watoto wote 7,719 wanaotarajiwa kuanza shule mwaka 2023, wanawasili shuleni. "Tumeweka jitihada za uandikishwaji wa shule za awali na msingi kwa kwa kuhimiza mabalozi na wenyeviti wa Mitaa kutembea nyumba kwa nyumba kuhakikisha kila mtoto anayestahili kwenda shule anakwenda" 

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kongwa White Zuberi amesisitiza suala la elimu kwa kusema; "Tumetumia fedha za Madarasa kujenga shule mbili ikiwemo hii ya Ihanda, Mhe. Rais anawasaidia watu wa chini kuweza kusoma mpaka ngazi ya juu kwa kutoa elimu bure kuanzia awali hadi kidato cha sita, hivyo tuunge mkono juhudi za Rais kwa kupeleka watoto shule"

Kwa upande wa sekta ya mazingira, Senyamule ameendelea kuhimiza kampeni yake aliyoizindua Desemba 31 mwaka Jana kwa kuwataka wanakongwa kupanda miti ya kutosha na kutunza vyanzo vya maji pia kuepuka ukataji miti holela. 

Sambamba na hilo, alionyesha mfano kwa kupanda Miti kwenye eneo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo pamoja na eneo la shule ya Sekondari Ihanda kama ishara ya kusisitiza wananchi kupanda miti na akasisitiza Wilaya hiyo kuhakikisha inafikia lengo la agizo la Serikali la kila Halmashauri kupanda miti 1,500,000 kwa mwaka.

Vilevile katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa alitembelea mradi wa ujenzi wa kituo mahiri cha nafaka  kilichopo eneo la Mtanana ambacho kitakua na utaalamu wa kuzuia sumu kuvu kwenye mazao. Mradi huu upo chini ya Wizara ya Kilimo na unagharimu takribani kiasi cha Shilingi Bilioni 19.

"Nimepata taarifa kituo hiki ni kikubwa Afrika Mashariki na kati, kitawezesha mazao yetu kuuzika kimataifa. Nimefarijika kusikia kuwa kituo hiki kitatoa mafunzo, hivyo naamini kitatoa darasa tosha. Naahidi sisi kama Mkoa, tutaendelea kusimamia mradi huu ili ukamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa" Amesema Senyamule.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa Omary Nkullo, amesema kujengwa kwa kituo hiki ni kutokana na historia iliyotokea miaka mitano iliyopita ambapo Mkoa ulipata vifo vya watu na wanyama kutokana na kula sumu kuvu kwenye mazao hivyo Wizara iliandaa mpango wa kutafuta eneo kwa ajili ya ujenzi na eneo hili tulihamisha wananchi kwa fidia ya Shilingi Milioni 8 hadi 9 na hati ya umiliki ikakabidhiwa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki.

 

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.