• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yasisitiza matumizi ya Teknolojia katika ulinzi na ufuatiliaji mienendo ya Wanyamapori

Imewekwa tarehe: October 15th, 2022

SERIKALI Kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itaendelea kutumia teknolojia ya kufuatilia mienendo ya wanyamapori katika maeneo ya hifadhi kwa kuwa imesaidia kwa kiasi kikubwa katika kutambua mienendo ya wanyamapori mbalimbali wakiwemo wale walio hatarini kutoweka na wanaosababisha migogoro kwenye jamii.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Morogoro na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alipokua akizindua zoezi la Kuvisha Mikanda yenye Redio za Mawasiliano kwa wanyamapori linalofanywa na Watalaam kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) lililofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ambapo jumla ya makundi 53 ya wanyamapori yanatarajiwa kifungwa mikanda hiyo nchi nzima.

Katika kufuatilia mienendo ya wanyamapori waliohatarini kutoweka, teknolojia hii husaidia kutambua uwepo wao, mienendo na mtawanyiko katika mifumo ikolojia yao. Utambuzi huu husaidia katika kuimarisha nyanda za malisho na ulinzi" amesema Balozi Dkt. Chana. 

Amesema kwa upande wa wanyamapori waharibifu, teknolojia hiyo husaidia kutambua makundi na mienendo yao na kutoa taarifa mapema kuhusu uwepo wa makundi hayo nje ya hifadhi na kichukua hatua kabla ya hayajasababisha madhara. 

"Taarifa hizi husaidia katika kupanga mbinu muafaka za kukabiliana na wanyamapori hao" amesisitiza Balozi Dkt. Chana. 

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa zoezi hilo alilolizindulia limelenga kuimarisha uhifadhi na utalii kusini mwa Tanzania hususan katika Hifadhi za Taifa za Nyerere, Ruaha na Mikumi akifafanua kuwa litasaidia kwa kiwango kikubwa katika kupunguza migogoro baina ya jamii zinazozunguka hifadhi.  "Jumla ya makundi ya wanyamapori 53 yatafungwa mikanda hii yenye redio za mawasiliano katika hifadhi hizi tatu." amesisitiza Balozi, Dkt. Chana.

Sambamba na hayo, Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameongeza kuwa wanyamapori watakaofungwa mikanda hiyo ni pamoja na makundi ya tembo, simba, chui, duma, mbwa mwitu na twiga. 

Aidha, taarifa na takwimu hizo zitasaidia kuandaa ramani za mitawanyiko ya wanyamapori katika misimu na nyakati mbalimbali ambazo zitasaidia kufungua njia mpya za utalii “tourism circuits” pamoja na kuimarisha uhifadhi wa wanyamapori katika hifadhi hizo.

Naye Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka amesema Tekinolojia hiyo itasaidia kuwalinda Wanyamapori na Hifadhi zetu hapa nchini. Pia, itasaidia kufuatilia mienendo ya Wanyamapori hai na kuweza kuwaona kidijitali pindi wanapotaka kuleta madhara.

"Kwa kutumia tekinolojia hii tunaweza kuwaona kidijitali wanapotembea na hasa wanapokaribia maeneo hatarishi ya kuleta madhara kwa wananchi"

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.