SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania rasmi imesitisha kupanda kwa bei mpya ya mafuta iliyoanza kutumika tarehe 1 Septemba baada ya kutangazwa na Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
EWURA ilitangaza bei hizo mpya na baadae kubadilisha bei hizo Akitoa ufafanuzi juu ya sakata hilo Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msingwa amaesema kuwa "Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliona kuna haja ya kuziangalia upya bei hizi..., na wakati zoezi hilo la kuangalia likifanyika, aliagiza ama alielekeza kwamba bei zilizotumika mwezi uliopita yaani za mwezi Agosti ndizo ziendelee...na hivi ninavyozungumza bei zinaendelea zile za mwezi Agosti. Zilizotangazwa kuanza tarehe 1 Septemba zimesitishwa na. Watanzania wanaendelea kutumia bei hizo za mwezi Agosti."
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.