WAZIRI wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameidhinisha shilingi bilioni 207 kwa ajili ya kuhakikisha maji salama yanapatikana Vijijini.
Pia amesema kuwa Bunge la Bajeti limepitisha kiasi cha shilingi bilioni 680 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji mijini na vijijini. Ameyasema hayo alipokuwa anaongea na Wawakilishi pamoja Wahariri wa Vyombo vya Habari Jijini Dodoma.
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema kuwa upatikanaji wa Maji kwa Jiji la Dodoma umeendelea kuimarika ambapo ameeleza kuwa japo bado uhitaji wa maji ni mkubwa, uzalishaji umeongezeka kutoka lita milioni 61.5 hadi kufikia lita milioni 66. Alisema kuwa uhitaji ni lita milioni 103 hali hii imesababishwa na ongezeko kubwa la watu kutokana na kuwepo kwa Makao Makuu ya Serikali mara mbili zaidi na ilivyokuwa mwaka 2015.
“Zipo jitihada ambazo Wizara hiyo imefanya kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) kwa kuchimba visima vikubwa vitatu Mzakwe na vingine maeneo ya pembezoni na kujenga tanki kubwa eneo la Buigiri, Chamwino huduma ya maji inapatikana kwa uhakika". amesema.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph amewatoa wasiwasi wakazi wa Jiji la Dodoma kuwa Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya maji itahakikisha inatatua kero zote za maji kwa kufanikisha miradi yote ambayo inaendelea kutekelezwa.
"Mradi wa kutoa maji Ihumwa kwenda tanki la Njedengwa umefikia asilimia 96 na kufikia mwezi Oktoba mwishoni utakuwa umekamilika na Wananchi wa maeneo Nzuguni, Kisasa, Mwangaza mpaka soko la Job Ndugai yatapata maji ya kutosha," amesema Mhandis Joseph.
Kazi ya kulaza mabomba ya inchi 10 line ya kusambazia maji inaendelea eneo la Mwangaza Fieldforce na mradi huu utahudumia maeneo Mwangaza, Kisasa, Nyumba 300, Ihumwa, Njedengwa, Nzuguni, Stand mpya na Soko la Job Ndugai.
Mradi huu wa Ihumwa - Njedengwa unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba 2021.
Mafundi wakiendelea na kazi ya kulaza mabomba ya inchi 10 line ya kusambaza maji maeneo ya Mwangaza.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.