SERIKALI imewasilisha Bungeni Makadirio ya Bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2021/2022 huku ikianisha Maeneo ya vipaumbele kwa Mwaka huo wa Fedha.
Akiwasilisha Makadirio hay oleo June10 Mwaka2021 Waziri wa Fedha na Mipango,Dk.Mwigulu Nchemba amesema kuwa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/22 ni ya kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya “Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu”. Bajeti hii itajielekeza katika utekelezaji wa vipaumbele mbalimbali.
“Vipaumbele vilivyoainishwa katika maeneo matano ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22,Maeneo hayo ni Kuchochea uchumi shindani na shirikishi; kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo; kukuza uwekezaji na biashara; kuchochea maendeleo ya watu; na kuendeleza rasilimali watu.
Waziri Mwigulu ameeleza kuwa ili kuwa na uchumi shindani na shirikishi, Serikali itajielekeza katika kugharamia miradi ambayo itajikita katika: Kujenga jamii yenye uwezo wa kushindana kikanda na kimataifa; kusimamia utulivu wa viashiria vya uchumi kwa ujumla.
Amefafanua kuwa kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji,kuchochea uvumbuzi na uhawilishaji wa teknolojia kutoka nje na kuendeleza miundombinu na huduma za reli, barabara za kufungua fursa za kiuchumi, kuunganisha nchi jirani, kupunguza msongamano mijini na barabara za vijijini, madaraja, usafiri wa majini na angani, mageuzi ya TEHAMA pamoja na kutekeleza mradi wa Tanzania ya Kidijitali, nishati, bandari na viwanja vya ndege. Eneo hili limetengewa jumla ya shilingi trilioni 7.44 ikijumuisha shilingi trilioni 3.13 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kielelezo.
Pamoja na mambo mengine ameitaja miradi mingine ya kielelezo itakayotekelezwa ni: Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL); Makaa ya Mawe – Mchuchuma na Chuma – Liganga ikijumuisha ujenzi wa reli ya kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay na matawi ya Mchuchuma na Liganga; Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania); Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) – Lindi; Mradi wa Kufua Umeme wa Maji – Ruhudji MW 358.
“ Mradi wa Kufua Umeme wa Maji – Rumakali MW 222; Uchimbaji wa madini ya Nickel; Ujenzi wa Madaraja Makubwa na Barabara za Juu za Daraja la Kigongo – Busisi (Mwanza), Tanzanite (Dar es Salaam) na Interchange ya Kamata (Dar es Salaam); Bandari ya Uvuvi (Mbegani) na Ununuzi wa Meli za Uvuvi; Kiwanda cha Sukari Mkulazi; Utafutaji wa mafuta katika vitalu vya Eyasi Wembere na
Mnazi Bay North; Mradi wa Magadi Soda – Engaruka; Kuongeza Rasilimali Watu yenye Ujuzi Adimu na Maalumu (Ujuzi wa Kati na Wabobezi) kwa Maendeleo ya Viwanda na Ustawi wa Jamii; na kuendeleza Kanda Maalumu za Kiuchumi. “,Amesema
Amesema kuwa katika eneo la kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma, msukumo utawekwa kwenye miradi ya viwanda inayolenga kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. Katika eneo hili, kipaumbele ni pamoja na: Kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji na uhifadhi wa mazao ya kilimo; kuimarisha vituo vya utafiti na huduma za ugani;
kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi; kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi; kuboresha huduma za uhimilishaji mifugo; na kujenga machinjio ya kisasa na minada ya mifugo.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaweka mkazo kwenye ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani ya madini pamoja na kuzalisha bidhaa zitakazotumia malighafi na rasilimali zinazopatikana nchini. Aidha, Bajeti hii itajielekeza katika kugharamia miradi na programu inayolenga kuboresha huduma za utalii, fedha na bima pamoja na kuendeleza viwanda vya uzalishaji wa dawa muhimu na vifaa tiba. Jumla ya shilingi trilioni 1.38 zimetengwa kugharamia utekelezaji wa miradi katika eneo hili.
Mheshimiwa Spika, katika eneo la kukuza uwekezaji na biashara, Serikali itagharamia programu zitakazoimarisha masoko ya ndani na kutumia fursa za masoko ya kikanda na kimataifa katika kukuza biashara. Masoko yanayolengwa ni yale yatakayotoa fursa kwa bidhaa zinazozalishwa nchini, ikiwemo bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu. Vilevile, Serikali
itaendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji ikiwemo kuendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Biashara na Uwekezaji (Blueprint). Eneo hili limetengewa jumla ya shilingi bilioni 31.6.
Dk. Nchemba amebainisha kuwa katika kuchochea maendeleo ya watu, miradi itakayotekelezwa italenga kuboresha maisha ya watu kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwemo elimu na mafunzo kwa ujumla, afya na ustawi wa jamii, huduma za maji na usafi wa mazingira na kinga ya jamii ikijumuisha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF. Aidha, Serikali itaendelea kupanga, kupima na kumilikisha ardhi mijini na vijijini, kusimamia na kuendeleza rasilimali za maji; na kuendelea na utekelezaji wa programu za kulinda mazingira na kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Jumla ya shilingi trilioni 4.43 zimetengwa.
katika jitihada za kuendeleza rasilimali watu, Serikali itagharamia programu inayolenga kuendeleza maarifa na ujuzi wa rasimali watu katika ngazi zote za elimu ikiwemo kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri.
Pia amesema Serikali itaendelea kuboresha viwango vya utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi pamoja na ujuzi adimu kwa lengo la kuongeza tija na ushindani wa wananchi katika kutumia rasimali zilizopo nchini ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii ambapo Jumla ya shilingi bilioni 50.5 zimetengwa.
Amesema Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 imeainisha kwa kina maeneo ya kipaumbele ambayo Serikali itayatekeleza kupitia Bajeti ya mwaka 2021/22.
pamoja na miradi ya kielelezo, Serikali itatekeleza miradi mingine ya uboreshaji wa miundombinu ambayo itagharamiwa na mikopo yenye masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia. Miradi hiyo ni Mradi wa Kuendeleza Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) wa kukabiliana na mafuriko kwenye Bonde la Mto Msimbazi utakaogharimu dola za Marekani milioni 120.
Mradi huu utahusisha ujenzi wa daraja katika eneo la Jangwani, na upanuzi na ujenzi wa kingo za mto Msimbazi. Mradi wa pili unahusisha uboreshaji wa barabara za kukuza fursa shirikishi za kijamii na kiuchumi ambapo Benki ya Dunia itatoa dola za Marekani milioni 300 na mchango wa Serikali ni dola za Marekani milioni 50. Mradi huu unalenga kuboresha barabara za vijijini katika maeneo yenye tija kubwa ya uzalishaji wa mazao ya kilimo.
katika hatua nyingine, Serikali imeanza mazungumzo na Benki ya Dunia kupitia dirisha la International Development Association (IDA) kwa ajili ya mradi wa uboreshaji miundombinu katika Majiji na Miji 45. Utekelezaji wa mradi huu utaanza katika mzunguko wa 20 (IDA 20) unaotegemewa kuanza Julai 2022 na utagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 500. Mradi utahusisha ujenzi wa miundombinu ya msingi ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa lengo la kukuza uchumi wa miji husika.
Amesema maeneo mengine muhimu ni pamoja na Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi Mwaka 2022ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajiandaa kufanya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu SURA 351.
“Kama mojawapo ya maandalizi ya utekelezaji wa Sensa ya Mwaka 2022 Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa upande wa Tanzania Bara na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar imekamilisha kuandaa Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka, 2022. Kitabu hiki kinaainisha namna ya usimamizi na utekelezaji wa zoezi zima la Sensa, gharama ya kufanya Sensa pamoja na muundo wa Sensa utakavyokuwa katika ngazi zote za kiutawala.”,amesema
Amesema jumla ya shilingi bilioni 328.2 zinatarajiwa kutumika kugharamia sensa ya mwaka 2022 na kwa mara ya kwanza katika historia ya Sensa nchini, Sensa ya Mwaka 2022 itatumia teknolojia ya vishikwambi (tablets) katika utengaji wa maeneo ya kijiografia na ukusanyaji wa takwimu uwandani. Matumizi ya teknolojia hii yana manufaa makubwa, hasa katika kupunguza gharama na muda wa kukusanya na kuchakata takwimu, hali inayowezesha kutoa matokeo ya Sensa ndani ya muda mfupi.
Amesema zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ni jukumu la kila mtu, natoa wito kwa kamati zote za Sensa, Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote, Waheshimiwa Wabunge pamoja na wananchi wote kwa ujumla kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha katika maandalizi ya Sensa na wajitokeze wote siku ya kuhesabu watu. Lengo ni kuhakikisha Watu waliolala nchini usiku wa kuamkia siku ya Sensa (usiku wa sensa) wanahesabiwa na kuchukuliwa taarifa zao za kiuchumi, kijamii, mazingira na makazi wanayoishi na mengine mengi kwa ajili ya kupanga mipango endelevu ya maendeleo ya wananchi.
Kuhusu maslahi ya Wafanyakazi Waziri huyo amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa watumishi wa umma na wa sekta binafsi katika kukuza Pato la Taifa Kwa kutambua hilo, Serikali itachukua hatua mbalimbali za kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira (PAYE) kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8.
Hatua hii ni mwendelezo wa juhudi za Serikali za kupunguza mzigo wa kodi kwa wafanyakazi, ambapo kiwango hicho kimepunguzwa kutoka asilimia 11 mwaka 2015/16 hadi asilimia 8 itakayoanza kutekezwa mwaka 2021/22 kwa Kufuta tozo ya silimia 6 iliyokuwa ikitozwa kwa ajili ya kulinda thamani ya mkopo wa elimu ya juu (Value Retention Fee) kwa wanufaika; na Kutenga jumla ya shilingi bilioni 449 kwa ajili ya kuwapandisha vyeo watumishi 92,619.
Akielezea kuhusu Maslahi ya Madiwani, Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata amesema kuwsa Madiwani wanafanya kazi nzuri za kusimamia shughuli za maendeleo kwenye Kata mbalimbali nchini ambapo wao ni wabunge wakaazi wa kwenye kata hizo ambao kila siku wako na wananchi katika kusimamia shughuli za maendeleo.
Hata hivyo, katika baadhi ya halmashauri madiwani wamekuwa wakikopwa posho zao, na wengine hufikia hatua ya kupiga magoti kwa wakurugenzi watendaji ili walipwe, hali hiyo imekuwa ikipunguza ufanisi katika halmashauri zetu kwa madiwani wengi kufanya maamuzi yanayopendekezwa na wakurugenzi watendaji hata kama hayana maslahi kwa Taifa ili waweze kulipwa posho zao.
“ Jambo hili limeongelewa kwa hisia kali sana na Waheshimiwa Wabunge hapa bungeni. Waheshimiwa Wabunge na Waheshimiwa Madiwani, napenda niwaeleze kuwa MAMA YETU amesikia kilio chenu na alinielekeza mimi pamoja na Waziri wa TAMISEMI kulitafutia ufumbuzi suala hili.”,
Waziri huyo amependekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho za kila mwezi za Waheshimiwa Madiwani moja kwa moja tena kwenye akaunti zao kwa Halmashauri zote zenye uwezo mdogo kimapato. Halmashauri 16 zenye uwezo mkubwa wa kimapato (Daraja A) zitaendelea kutumia mapato yake ya ndani kulipa posho za Madiwani kupitia kwenye akaunti zao.
Kwa upande wa Maafisa Tarafa ambao ni viunganishi muhimu wa ngazi za kata na Wilaya zetu ambapo wengi wao hufanya kazi nzuri sana ya kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya Serikali katika maeneo yao. Kwa kutambua umuhimu wao, Serikali ya CCM iliwapatia pikipiki viongozi hawa ili waweze kufanya kazi zao vizuri.
Hata hivyo, wengi wao wanashindwa kugharamia ununuzi wa mafuta na matengenezo ya vitendea kazi hivi na kulazimika kuwachangisha wananchi na hata wengine kuomba msaada kwa wadau mbalimbali. Hali hii inapunguza sana ufanisi katika Tarafa zetu. Kupitia hotuba hii, napenda niwajulishe Maafisa Tarafa wote nchini kuwa MAMA YETU amesikia kilio chenu. Hivyo, napendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho ya shilingi 100,000/= kwa mwezi kwa kila Afisa Tarafa ili waweze kumudu gharama za mafuta na matengenezo ya pikipiki.
Waziri Nchemba amesema Watendaji Kata ndio wasimamizi wa kazi za sekta zote na ni watendaji wakuu kwenye kata. Wengi wao wanafanya kazi katika mazingira magumu ili kufanikisha shughuli za maendeleo katika kata zetu ikiwemo kusimamia ukusanyaji wa mapato na masuala ya usalama. Idadi kubwa ya watendaji hawa hutumia mishahara yao kufanya kazi mbalimbali ikiwemo ufutiliaji wa mapato ya Serikali kwa kukodi pikipiki ili kufanikisha shughuli zilizopo.
“ Kwa ujumla wanafanya kazi nzuri sana ya kusimamia shughuli za maendeleo kwenye kata zetu. Jambo hili limeongelewa kwa hisia kali sana na Mheshimiwa Rose Busiga, Mbunge wa Viti Maalum (Geita), ambaye ni mtendaji wa kata mstaafu na kuungwa mkono na wabunge wengi hapa bungeni. Waheshimiwa wabunge, MAMA YETU amesikia kilio hiki na kutuelekeza kulitafutia ufumbuzi suala hili. Hivyo, napendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali kuanza kulipa posho ya shilingi 100,000/= kwa mwezi kwa kila Mtendaji Kata kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri yaliyokuwa yakitumika kulipa madiwani.”amesema
Kuhusu Madeni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii amesema wastaafu walilitumikia Taifa kwa uzalendo, uadilifu na bidii kubwa hivyo hawawezi kuhesabu mafanikio ya nchi bila kutaja mchango wa wazee hao.
Amefafanua kuwa Kumekuwepo na changamoto za muda mrefu za ulipaji wa mafao yao kutokana na ufanisi mdogo wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika kuhudumia wastaafu ambapo hali hiyo kwenye mifuko imechangia uwepo wa madeni ambayo mifuko inaidai Serikali na hivyo kusababisha wastaafu wetu kukosa au kusubiri kwa muda mrefu ili kulipwa mafao yao.
“Jambo hili pia limejadiliwa kwa hisia kali na Waheshimiwa Wabunge hapa bungeni. Wazee wetu hawa hupata shida sana, ambapo baadhi yao hufadhiliwa malazi kwa kulala misikitini na makanisani na wengine hutegemea wahisani kuhudumia familia zao kinyume na mchango walioutoa katika ujenzi wa nchi hii. MAMA YETU amesikia kilio cha wazee hawa na kutuelekeza Wizara ya Fedha na Mipango kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kukamilisha zoezi la kitaalamu ili kujua hali halisi ya madeni na namna bora ya kulipa madeni hayo.”,
Aidha amependekeza kulipa madeni yanayodaiwa na mifuko kwa kutenga fedha kwenye bajeti na kutumia utaratibu wa kutoa hatifungani maalum isiyo taslimu (Non cash Special Bond) zitakazoiva kwa nyakati tofauti kuanzia miaka miwili hadi 25.
Amesema Utaratibu wa hatifungani una faida mbalimbali zikiwemo: kuipa Serikali nafasi ya kibajeti ya kuendelea kutekeleza miradi mingine ya maendeleo; kuiwezesha Serikali kuyatambua madeni hayo kwenye kanzidata ya madeni; na kuzuia madeni hayo kuendelea kuongezeka kulingana na tathmini ya thamani ya madai (actuarial valuation).
Aidha, utaratibu huo utaboresha mizania ya hesabu na mtiririko wa mapato yanayotokana na riba ya hatifungani hizo kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Hatua hii inakwenda kumaliza kabisa tatizo hilo la wazee wetu kudai haki yao kwa damu na machozi yaliyodumu kwa muda mrefu.
Amesema Serikali imepokea malalamiko kuhusu kucheleweshwa kwa michango ya watumishi kupelekwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na baadhi ya ofisi za Serikali kutopeleka kabisa michango hiyo na Jambo hilo llimekuwa likisababisha usumbufu kwa watumishi punde wanapostaafu.
Sambamba na hilo amependekeza kulipa michango hiyo moja kwa moja kutokea Hazina kwa taasisi zote ambazo watumishi wanalipwa na Hazina. Taasisi ambazo zinalipa watumishi kutokana na vyanzo vyao vya mapato zitaendelea kupeleka michango ya watumishi wao kwa ufuatiliaji wa karibu wa Serikali. Serikali itafanya uhakiki na kulipa madeni ya michango ambayo haijawasilishwa kwenye mifuko hadi sasa.
Kuhusu jeshi la polisi askari wapiganaji, kuna utaratibu wa wapiganaji kufanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi kwa miaka 12 kabla hawajapata ajira za kudumu. Jambo hili huwasababishia wapatapo mkataba wa kudumu wawe wamechelewa kwa miaka 12 ikilinganishwa na mtumishi mwingine aliyeingia pamoja kazini katika idara nyingine. Jambo hili linamadhara hasi katika itifaki ya utumishi na mafao ya mpiganaji
anapostaafu.
“ Hiki kimekuwa kilio cha muda mrefu cha askari wa Jeshi la Polisi. Kutokana na changamoto hiyo, MAMA YETU amesikia kilio cha askari hao na alituelekeza tukae na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kutafuta suluhisho la jambo hili. Napendekeza kuanzia mwaka 2021/22 askari wa Jeshi la Polisi wataingia mkataba wa kipindi cha miaka 6 na kuingia katika ajira ya kudumu.
Aidha amesema Kurahisisha Kasi ya Utekelezaji wa Miradi katika kuimarisha usimamizi na ufanisi katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango itafanya mabadiliko katika Kanuni ya 21 ya Sheria ya Bajeti, SURA 439 ili kuondoa changamoto iliyopo ya fedha ambazo hazijatumika hadi tarehe 30 Juni kila mwaka kurejeshwa Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.
Amesema Mabadiliko hayo yatatoa fursa kwa Maafisa Masuuli kuwasilisha taarifa ya fedha kuvuka mwaka hadi tarehe 30 Juni kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali badala ya siku 15 kabla ya mwaka wa fedha kumalizika. Fedha hizo zitawekwa kwenye Akaunti ya Amana kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli ambazo hazijakamilika wakati wa utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha husika.
Kwa msingi huo, kuanzia sasa hakutakuwa na fedha zenye miadi zitakazorejeshwa Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ifikapo tarehe 30 Juni ya kila mwaka wa fedha isipokuwa pale ambapo Maafisa Masuuli wamekiuka masharti ya Sheria ya Bajeti, SURA 439 na Sheria ya Fedha za Umma, SURA 348.
Kuhusu kodi ya Majengo amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika ukusanyaji wa kodi ya majengo, hali iliyosababisha Serikali kubadili njia za ukusanyaji mara kwa mara. Kabla ya mwaka 2017/18, Serikali za Mitaa zilikuwa na jukumu la kukusanya mapato hayo lakini hazikufanya vizuri.
Ameeleza kuwa Kuanzia mwaka 2017/18, Serikali ilitumia Mamlaka ya Mapato kukusanya kodi hiyo, ambapo pia haikufanya vizuri. Ukusanyaji wa kodi hii kwa kutumia Serikali za Mitaa au TRA umekuwa ukitumia njia za kizamani ambazo zinahusisha watu kusafiri, kupanga foleni na kukusanya fedha taslimu (cash).
Utaratibu huu unatumia gharama kubwa, muda na ni hatarishi kwa mapato. Katika kuhakikisha kodi hii inafikia malengo, Serikali imeandaa utaratibu mzuri wa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi ya majengo.
Kwa upande wa Kodi ya Wajasiliamali,Waziri huyo amesema wafanyabiashara na watoa huduma wadogo nchini wameendelea kutambulika kupitia vitambulisho vya wajasiriamali. Tangu kuanza kwa zoezi la utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara na watoa huduma wadogo nchini, jumla ya vitambulisho 2,335,711 vimegawiwa ambavyo vimewezesha kukusanya jumla ya shilingi bilioni 46.71.
“ Lengo ni kuendelea kuwatambua wafanyabiashara wadogo na kuwawekea mazingira rafiki ya ufanyaji biashara. Katika mwaka 2020/21, Serikali imefanya maboresho ya vitambulisho hivyo kwa kuweka picha na jina la mjasiriamali ili kuongeza udhibiti na kufungua fursa kwa wajasiriamali kuweza kutumia vitambulisho hivyo kupata huduma za kibenki na bima ya afya. Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea na uratibu wa kugawa vitambulisho hivi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania ambayo ndiyo yenye mfumo wa kusajili wafanyabiashara hao, kuchapisha vitambulisho na kuwapatia Halmashauri husika kwa ajili ya kugawa. “,
Kuhusu Maboresho ya mfumo wa kodi, ada na tozo mbalimbali amewasilisha mapendekezo ya kufanya marekebisho ya mfumo wa kodi, ikiwemo baadhi ya viwango vya kodi, tozo na ada zinazotozwa chini ya Sheria mbalimbali na kurekebisha taratibu za ukusanyaji na usimamiaji wa mapato ya Serikali.
Marekebisho haya yamezingatia dhamira ya Serikali ya kurejesha ukuaji wa uchumi katika hali ya kawaida baada ya athari zilizotokana na UVIKO-19 sambamba na kuendelea kuwa na mfumo wa kodi ambao ni tulivu na wa kutabirika ili kuvutia uwekezaji kutoka ndani na nje. Vile vile, marekebisho yanalenga kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi hususan katika sekta ya kilimo na viwanda, kuongeza kipato kwa waajiriwa na kuongeza mapato ya Serikali.
Aidha, Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Kufanya Biashara (BluePrint) kwa kuwianisha tozo na ada mbalimbali zinazotozwa na Wizara na Mamlaka za Udhibiti kwa lengo la kupunguza na kurahisisha ulipaji wake au kuzifuta baadhi ya tozo na ada hizi. Marekebisho yanayopendekezwa yanahusu Sheria zifuatazo:
(a) Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148; (b) Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 3
(c) Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147(d) Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004; (e) Sheria ya Usimamizi wa Kodi, SURA 438;
(f) Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, SURA 290; (g) Sheria ya Kodi ya Majengo, SURA 289;
(h) Sheria ya Ardhi, SURA 113;
(i) Sheria ya Ushuru wa Stempu, SURA 189;
(j) Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82; (k) Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, SURA 41;
(l) Sheria ya Ukaguzi wa Umma, SURA 418;
(m) Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, SURA 134 (n) Sheria ya Usajili wa Magari, SURA 124;
(o) Sheria ya Usalama Barabarani, SURA 168;
(p) Sheria ya Raia wa Kigeni (Uratibu wa Ajira) Na. 1 ya mwaka 2015;
(q) Marekebisho ya Ada na Tozo mbalimbali zinazotozwa na Wizara, Mikoa Wakala, Mamlaka za Udhibiti na Idara zinazojitegemea;
(r) Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya Sheria za Kodi na Sheria nyingine mbalimbali;
(s) Kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Kufanya Biashara (Blueprint) kwa kurekebisha Ada na Tozo mbalimbali;
(t) Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta, SURA 220; (u) Sheria ya Petroli, SURA 392; na
(v) Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, SURA 306.
27
Kwa upande wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148 amependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148 kama ifuatavyo(i) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye vyumba vya ubaridi (cold rooms) vinavyotambuliwa kwa H.S Code 9406.10.10 na 9406.9010. Lengo la msamaha huu ni kuwapunguzia gharama wazalishaji wa mbogamboga na maua nchini ili kuchochea kilimo cha kisasa,Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye madini (precious metals) na makinikia yatakayoingizwa nchini kwa ajili ya kuchenjuliwa, kuongezewa thamani na kuuzwa kwenye masoko ya madini yanayotambulika nchini. Lengo la pendekezo hili ni kuviwezesha viwanda vya uchenjuaji vilivyoanzishwa nchini kupata malighafi ya kutosha kwa ajili ya uchakataji na hatimaye kuongeza ajira na mapato ya Serikali;
Mapendekezo mengine ni Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye huduma za bima ya mifugo ambapo Lengo la marekebisho haya ni kuchochea shughuli za ufugaji nchini ikiwemo Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa na huduma zitakazoingizwa au kununuliwa hapa nchini kwa ajili ya kutekeleza mradi wa mafuta ghafi (EACOP).
Lengo la marekebisho haya ni kutoa unafuu wa kodi katika utekelezaji wa miradi tajwa;
(v) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye mafuta ghafi yanayotambulika kwa H.S Code 2709.00.00 kwa lengo la kutoa unafuu kwa mlaji ikiwemo Kampuni ya uendeshaji wa bomba la mafuta (EACOP)Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye Nyasi Bandia zinazotambulika kwa HS Code 5703.30.00 na 5703.20.00 kwa ajili ya Viwanja vya Mpira vilivyoko kwenye Majiji. Msamaha huo utahusisha ridhaa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania. Lengo la hatua hii ni kuendeleza michezo na kukuza vipaji nchini.
Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye kadi za kutengeneza vitambulisho vya taifa zinazotambulika kwa H.S Code 3921.11.90.00 na malighafi nyingine za kutengeneza kadi hizo zinazotambulika kwa H.S Code 3921.11.90.00 zitakazoingizwa nchini na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Lengo la pendekezo hili ni kupunguza gharama za kutengeneza Vitambulisho vya Taifa na kuharakisha upatikanaji wake.
Amesema Kumekwepo na ukiritimba katika kupokea fedha za misaada kwenye miradi ya maendeleo kwa hitaji la kisheria la kusubiri idhini ya Baraza la Mawaziri likae ili kuidhinisha misamaha. Napendekeza Kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa Taasisi zisizo za kiserikali (NGO’s), kwenye bidhaa na huduma zitakazotumika kwenye miradi inayotekelezwa na taasisi husika. Aidha, taasisi zitakazonufaika na msamaha huo ni zile ambazo zina mikataba na Serikali yenye kipengele kinachotoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani.
Pia amesema Sekta ya mawasiliano imekuwa ikikua vizuri na kuwa kiungo muhimu cha kuongeza wigo wa wananchi ambao wako kwenye ulimwengu wa kidijitali na kwenye sekta ya fedha (Financial Inclusion). Napendekeza kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye simu janja za mkononi (smart phones) HS Code 8517.12.00, vishikwambi (Tablets) HS Code 8471.30.00 au 8517.12.00 na modemu (modems) HS Code 8517.62.00 au 8517.69.00. Lengo la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya huduma za mawasiliano ili kufikia lengo la asilimia 80 ya watumiaji wa intaneti ifikapo mwaka 2025 kutoka asilimia 46 iliyopo sasa.
Amesema mapendekezo mengine ni Kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye mikebe inayotumika kuhifadhia maziwa inayotambuliwa kwa H.S Code 7310.29.20 ambayo kwa sasa haitumiki kwa ajili ya kazi hiyo na badala yake napendekeza kutoa msamaha wa kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye mikebe ya kubebea maziwa inayotambulika kwa H.S Code 7310.29.90, 7310.10.00 na 7612.90.90. Lengo la Pendekezo hili ni kuwapunguzia gharama wazalishaji na kuchochea ukuaji wa sekta ya maziwa nchini;
‘’Kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye taa zinazotumia umeme wa jua zinazotambulika kwa H.S. Code 85.13 na 94.05. Lengo la pendekezo hili ni kuwianisha msamaha huu sambamba na msamaha unaotolewa chini ya Sheria ya Ushuru wa Forodha ambayo inasamehe Kodi kwenye vifaa vinavyotumika kuzalisha nishati ya umeme wa jua pekee na kurahisisha usimamizi wake. Aidha, pendekezo hili linalenga kuweka usawa katika ulipaji kodi kwa watumiaji wa taa zinazotumia nishati za aina zote’’
Amesema kuwa Kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha asilimia sifuri kwenye huduma ya usafirishaji na huduma zinazohusiana na usafirishaji wa mafuta ghafi kupitia bomba linalojengwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Tanzania na Uganda (EACOP).
Amesema kuwa Lengo la pendekezo hilo ni kuwezesha huduma tajwa kutekelezwa bila kodi sanjari na uzoefu wa kimataifa kwa bidhaa zilizopita hapa kwenda nchi jirani au ng’ambo kwa
kuzitambua bidhaa za mtaji zilizomo kwenye Sura ya 84, 85 na 90 ya Kitabu cha Ushuru wa Pamoja wa Forodha wa Afrika Mashariki kuwa bidhaa za mtaji zitakazostahili kupata kivutio cha ahirisho la malipo ya VAT.
Amesema kuwa Lengo la pendekezo hilo ni kuwianisha maana ya bidhaa za mtaji kwenye Sheria za kodi na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali kwenye Kubadilisha utaratibu wa kutoa msamaha kwenye miradi ya Serikali inayogharamiwa na fedha za serikali na fedha za wafadhili ambapo mnufaika wa msamaha huo atawasilisha maombi kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania badala ya utaratibu wa kuwasilisha kwa Waziri wa Fedha kwa ajili ya kupata ridhaa na kutoa Tangazo la Serikali (GN) kwa kila mradi.
‘’Utaratibu huu utarahisisha na kuharakisha utoaji wa misamaha badala ya utaratibu wa sasa kutokana na TRA kuwa na ofisi kwa kila mkoa nchini kote ambazo zinaweza kupokea, kuchambua na kusimamia matumizi sahihi ya misamaha’’amesema
(Kuhusu Zanzibar, Waziri huyu amependekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kurudisha utaratibu wa kurejesha VAT kwa bidhaa zinazonunuliwa Tanzania Bara na kutumika Tanzania Zanzibar. Hii inatokana na mfumo wa kutoza VAT kwa kiwango cha asilimia sifuri kwa bidhaa za viwandani pekee kutowanufaisha wafanyabiashara wa Zanzibar wanaonunua bidhaa na kutozwa VAT Tanzania Bara na kutozwa tena VAT bidhaa hizo zinapopelekwa Zanzibar.
Aidha, amependekeza marejesho ya VAT yatakayofanyika kwa bidhaa zinazotoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar yafanyike pia kwa bidhaa zitakazotoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara sambamba na marekebisho ya vifungu husika vya Sheria za VAT kwa pande zote mbili za muungano. Ili kuwa na ufanisi wa marejesho, maboresho ya mifumo yatafanyika ili isomane baina ya Tanzania Bara na Zanzibar. Kutokana na utaratibu huu, kiwango cha asilimia sifuri ya Kodi ya Ongezeko la Thamani kilichokuwa kinatozwa bidhaa hizo kitasitishwa.
Amesema kuwa kutokana na hatua zote za Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa ujumla zinatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 55,499.97.
Kuhusu Sheria ya Kodi ya Mapato,Waziri amependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato, Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza Kodi ya Mapato yanayohusiana na ajira kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8.
Waziri huyu amesema kuwa jumla ya Mapato Kiwango cha Kodi sasa
Mapato ya jumla yasiyozidi shilingi 3,240,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 3,240,000/= lakini hayazidi
shilingi.6,240,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 6,240,000/= lakini hayazidi shilingi 9,120,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 9,120,000/= lakini hayazidi shilingi 12,000,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 12,000,000/=
Jedwali Na. 1B Viwango vinavyopendezwa
Mapato ya jumla yasiyozidi shilingi 3,240,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 3,240,000/= lakini hayazidi shilingi 6,240,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 6,240,000/= lakini hayazidi shilingi 9,120,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 9,120,000/= lakini hayazidi shilingi 12,000,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 12,000,000/=
Hakuna kodi
9% ya kiasi kinachozidi shilingi 3,240,000/=
Shilingi 270,000/= jumlisha 20% ya kiasi kinachozidi shilingi 6,240,000/=
Shilingi 846,000/= jumlisha 25% ya kiasi kinachozidi shilingi 9,120,000/=
Shilingi 1,566,000/= jumlisha 30% ya kiasi kinachozidi shilingi
12,000,000/=
Hakuna kodi
8% ya kiasi kinachozidi shilingi 3,240,000/=
Shilingi 240,000/= jumlisha 20% ya kiasi kinachozidi shilingi 6,240,000/=
Shilingi 816,000/= plus 25% ya kiasi kinachozidi shilingi 9,120,000/=
Shilingi.1,536,000/= plus 30% ya kiasi kinachozidi shilingi
12,000,000/=
Pia amesema kuwa hatua hiyo inachukuliwa ikiwa ni dhamira ya Serikali ya muda mrefu kuwapunguzia mzigo wa Kodi wafanyakazi. Hatua hii inatarajiwa kupunguza mapato kwa shilingi milioni 14,178.06,kwa Kutoa msamaha wa Kodi ya Mapato kwenye hatifungani za Serikali. Sheria ya Kodi ya Mapato ilisamehe Kodi ya Mapato kwenye hatifungani kwa mwaka 2002/03 pekee. Lengo la hatua hii ni kuhakikisha soko la ndani la hatifungani linaendelea kusaidia kugharamia miradi ya Serikali.
Amesema kuwa kumekuwepo na ukiritimba katika kupokea fedha za kutoka kwa nchi wahisani zinazokwenda kutekeleza Miradi ya maendeleo. Napendekeza Kurejesha utaratibu wa Mamlaka ya Waziri mwenye dhamana ya Fedha kutoa msamaha kwa kutoa tangazo la Serikali (GN) bila sharti la kupata ridhaa ya Baraza la Mawaziri kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za wafadhili kupitia mikataba iliyoingiwa baina ya nchi hizo na Serikali yenye kifungu kinachoruhusu msamaha wa kodi ya mapato.
‘’ Lengo la marekebisho haya ni kuharakisha utekelezaji wa madi inayofadhiliwa kwa misaada na mikopo yenye gharama nafuu ambayo utekelezaji wake umekuwa ukichelewa kusubiri ridhaa ya Baraza la Mawaziri’’
Amesema kuwa Kutoza Kodi ya Zuio kwa kiwango cha asilimia mbili kwenye malipo yanayohusisha mauzo ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi yanapouzwa kwenye kampuni na mashirika yote yanayojihusisha na usindikaji na ununuzi wa mazao,Kwa sasa, Taasisi za Serikali pekee kama vile (Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ndizo zinakata kodi hiyo kwa kiwango cha asilimia mbili.
Aidha,amesema kuwa pendekezo hilo halitahusisha wakulima wadogo na wale wanaouza mazao yao kwenye masoko ya msingi (AMCOS) na kwenye magulio. Lengo la pendekezo hili ni kuweka usawa katika utozaji wa kodi kwa Kampuni zote zinazojishughulisha na mazao ya Kilimo, mifugo na uvuvi.Pendekezo hilo linatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 43,954.2;
(v) Kufanya maboresho ya Sheria ya Kodi ya Mapato ili kuwezesha ukokotoaji wa gharama za uchakavu kwa kiwango maalum cha asimilia tano (5) kwenye gharama za mali za ujenzi wa bomba la mafuta (EACOP). Lengo la pendekezo hili ni kuwianisha gharama za uchakavu na muda wa matumizi wa bomba husika kwa kuzingatia masharti ya mkataba uliosainiwa baina ya Serikali za Uganda na Tanzania;
(vi) Kuweka utaratibu maalum wa utozaji kodi kwa wachimbaji wadogo wa madini wenye mauzo ghafi yasiyozidi shilingi milioni 100 kwa mwaka kama ifuatavyo: –
(a) Kutoza kodi wachimbaji wadogo wa madini kwa kiwango mfuto cha asilimia 3 kwenye thamani ya mauzo ya madini pindi yanapopatikana;
(b) Kuweka muda wa ulipaji kodi kuwa ni wakati wanapouza madini na kulipa mrabaha kwenye Tume ya Madini au maeneo maalum yaliyoanzishwa chini ya sheria ya madini;
(c) Kuweka wajibu kwa mchimbaji mdogo wa madini kama mwajiri wa kukata kodi ya mapato ya ajira kutoka kwa wafanyakazi wake pale tu madini yatakapokuwa yamepatikana na kuuzwa katika masoko ya madini;
(d) Kuweka muda maalum wa kulipa kodi ya zuio ya ajira kuwa ni wakati mchimbaji mdogo anapouza madini na kulipa mrabaha katika masoko ya madini au vituo vingine vya uuzaji na ununuzi wa madini vinayotambuliwa na Tume ya Madini.
(e) Kuweka kiwango cha kodi cha mapato ya ajira (PAYE) cha asilimia 0.6 ya thamani ya mauzo ya madini ambayo italipwa na mwajiri (mchimbaji mdogo wa madini) kwa niaba ya wafanyakazi wake.
Amesema kuwa Lengo la mapendekezo hayo ni kurahisisha utozaji na ulipaji wa kodi kutoka kwa wachimbaji wadogo wa sekta ya madini ili kuongeza mchango wa kodi ya mapato kutoka kwenye sekta hiyo. Hatua hizi kwa pamoja zinatarajia kuongeza mapato ya Serikali shillingi
milioni 29,776.14
Kwa upande wa Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, amesema kuwa Kwa mujibu wa kifungu cha 124(2) cha Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, marekebisho ya viwango maalumu vya ushuru wa bidhaa (specific duty rates) kwa bidhaa zote zisizo za petroli yanaweza kufanyika kila mwaka ili kuvihuisha na mfumuko wa bei na viashiria vingine vya uchumi jumla.
Hata hivyo, kutokana na biashara za bidhaa hizi kuzorota kutokana na athari za kiuchumi zilizosababishwa na ugonjwa wa Covid-19, amependekeza kutofanya mabadiliko ya viwango maalumu vya ushuru wa bidhaa kwa bidhaa zote zisizo za petroli isipokuwa vinywaji vikali na bia zitakazotengenezwa kwa kutumia shayiri iliyozalishwa hapa nchini.
Amependekeza pia kufanya marekebisho ya Ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa kwa Kupunguza Ushuru wa Bidhaa kwenye bia zinazotengenezwa kwa kutumia shayiri iliyozalishwa hapa nchini kutoka shilingi 765 kwa lita za sasa hadi shilingi 620 kwa lita.
Lengo la mapendekezo hayo ni kuchochea kilimo cha shayiri hapa nchini kwa Kuanza kutoza Ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nyuzi na kamba za plastiki (synthetic fibres) zinazoingizwa kutoka nje ya nchi au kuzalishwa hapa nchini zinazotambuliwa kwa heading 55.11 na 56.07 isipokuwa zile zinazotumika kwenye
Uvuvi (HS Code 5607.50.00).
Marekebisho hayo ni kulinda mazingira na kuchochea uzalishaji na matumizi ya bidhaa za katani. Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa shilingi milioni 2,644
(iii) Kuanzisha tozo ya ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 10 kwenye pikipiki zilizotumika kwa zaidi ya miaka 3 zinazoingizwa nchini zinazotambuliwa kwa HS Code 8711. Lengo la marekebisho haya ni kudhibiti uingizaji wa pikipiki chakavu na kulinda mazingira. Hatua hii inatarajiwa kuongeza ya mapato ya Serikali kwa shilingi milioni 263.7.
Hatua za kutoza Ushuru wa Bidhaa kwenye bidhaa zisizo za petroli kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 2,907.7.
Kuhusu Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 Waziri huyu amesema katika Kikao cha Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki cha Maandalizi ya Bajeti kilichofanyika tarehe 7 Mei 2021 mjini Arusha, walipendekeza kufanya marekebisho ya Viwango vya Pamoja vya Ushuru wa Forodha na Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004) kwa mwaka wa fedha 2021/22.
Amesema kuwa Mapendekezo hayo yanalenga katika Kuboresha Maisha ya Watu Kupitia Maendeleo ya Viwanda na Kutengeneza Ajira kwa ajili ya Ustawi wa Pamoja wa Watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amesema kuwa mapendekezo ya Mawaziri wa Fedha ya kufanya marekebisho kwenye Viwango vya Pamoja vya Ushuru wa Forodha yanahusisha hatua mpya na zinazoendelea ambazo zimekuwa zikitekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2020/21.
Hatua hizo ni kama Mapendekezo ya hatua mpya za Viwango vya Ushuru wa Forodha ni Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye mabasi ya abiria yanayotambulika kwa HS Codes 8702.10.99 na 8702.20.99 yanayoingizwa nchini kwa ajili ya mradi wa mwendokasi. Hatua hii inalenga kupunguza gharama za uingizaji wa mabasi hayo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi;
(b) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye nyuzi za pamba (cotton yarn) zinazotambulika kwa Headings 52.05, 52.06 na 52.07. Lengo la hatua ni kulinda viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo na kuongeza thamani ya zao la pamba (value addition) nchini;
(c) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye matairi mapya ya pikipiki (new pneumatic tyres of rubber) yanayotambulika kwa HS Code 4011.40.00. Lengo la hatua ni kuongea mapato ya Serikali kwa kuwa matairi haya ni bidhaa zilizokamilika kwa ajili ya mtumiaji;
(d) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye siagi ya karanga (peanut butter) inayotambulika kwa HS Code 2008.11.00. Lengo la hatua ni kulinda wazalishaji wa bidhaa hiyo nchini;
(e) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye nyaya (wire of other alloy steel) zinazotambulika kwa HS Codes 7229.20.00 na 7229.90.00. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama kwa
Kuhusu wazalishaji wanaotumia bidhaa hiyo kama malighafi ni Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye milk cans zinazotambulika kwa HS Codes 7310.10.00 na 7310.29.90. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwenye sekta ya maziwa nchini;
(g) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye LABSA (Organic surface-active agents – Anionic) inayotambulika kwa HS Code 3402.11.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa sabuni za unga na maji nchini;
(h) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kuchakata ngozi zinazotambulika kwa HS Code 3208.20.00 na 3210.00.10 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa ngozi nchini;
(i) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kutengeneza mbolea zinazotambulika kwa HS Codes 2710.99.00, 2528.00.00 na 3505.20.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa mbolea nchini;
(j) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya
38
tumbaku iliyochakatwa vinavyotambulika kwa HS Code 5310.10.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa tumbaku nchini;
(k) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya chai iliyochakatwa vinavyotambulika kwa HS Codes 4819.20.90, 5407.44.00 na 3923.29.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa chai (tea blenders) nchini;
(l) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi ya kutengeneza masufuria ya aluminium inayotambulika kwa HS Code 7606.92.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa watengenezaji wa masufuria hayo nchini;
(m) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwa waunganishaji wa pikipiki za matairi matatu bila kujumuisha fremu kwa kuwa zinatengenezwa hapa nchini (CKD for three-wheel motorcycles excluding chassis and its components) zinazotambulika kwa HS Code 8704.21.90 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa waunganishaji wa pikipiki hizo nchini ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo;
(n) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kutengeneza mabomba ya plastiki (glass reinforced plastic pipes) zinazotambulika kwa HS Codes 3920.61.10, 7019.39.00, 7019.31.00, 6006.90.00, 7019.12.00,
3920.10.10, 4016.93.00, na 3907.91.00 kwa utaratibu wa duty remission.
Amesema kuwa Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa watengenezaji wa mabomba hayo nchini ili kupunguza gharama za uzalishaji na kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya maji; na
(o) Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwenye mabati (Flat-rolled products of other alloy steel, of a width of 600mm or more, not further worked than hot-rolled, in coils) yanayotambulika kwa HS Code 7225.30.00. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama kwa wazalishaji wanaotumia bidhaa hiyo kama malighafi.
(ii) Mapendekezo ya kuendelea na utekelezaji wa Viwango vya Ushuru wa Forodha vya mwaka 2020/21 ni kama ifuatavyo:
(a) Kupunguza Ushuru wa Forodha hadi asilimia 0 kutoka viwango vya awali vya asilimia 10 na asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi zinazotumika katika uzalishaji wa vifaa maalum vinavyotumika katika kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (UVIKO-19) vikiwemo Barakoa (Masks), kipukusi
(sanitizer), mashine za kusaidia kupumua (ventilators), na mavazi maalum ya kujikinga yanayotumiwa na madaktari na wahudumu wa afya (PPE). Msamaha huu utatolewa kwa utaratibu wa “duty remission”. Hatua hii inalenga kutoa unafuu wa uzalishaji wa vifaa hivyo hapa nchini ili kuongeza kasi katika kupambana na ugonjwa huo;
(b) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye mashine za kielektroniki zinazotumika kukusanya mapato ya Serikali (Cash registers, Electronic Fiscal Device (EFD) Machines and Point of Sale (POS) machines zinazotambulika katika HS Code 8470.50.00 na 8470.90.00. Lengo la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya vifaa hivi katika kuhasibu mapato ya Serikali;
(c) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vinavyotumiwa na wazalishaji wa maziwa kwa joto la juu yanayodumu kwa muda mrefu (UHT Milk) vinavyotambulika kwa HS codes 4819.50.00. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa maziwa hapa nchini. Utaratibu wa Duty Remission utakaotumika kutoa unafuu huo;
(d) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka kiwango cha asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifuniko vya chupa za mvinyo (corks and stoppers) vinavyotambulika kwa HS Codes 4503.10.00 kwa kuzingatia kuwa havizalishwi hapa nchini. Hatua hii inalenga kuwapunguzia gharama wazalishaji wa mvinyo ili kuhamasisha na kuendeleza kilimo cha zao la zabibu nchini pamoja na ajira. Utaratibu wa Duty Remission utakaotumika kutoa unafuu huo;
(e) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za marumaru zinazotambulika kwa HS Code 6907.21.00; 6907.22.00; na 6907.23.00 zinazoingizwa kutoka nje. Lengo la hatua hii ni kulinda na kukuza viwanda vya ndani vinavyozalisha marumaru pamoja na kuongeza ajira;
(f) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye chai inayotambulika kwa HS Code 09.02 inayoagizwa kutoka nje. Lengo la pendekezo hilo ni kulinda viwanda vya ndani na kuhamasisha kilimo cha chai hapa nchini pamoja na kuongeza ajira katika sekta ya kilimo;
(g) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye magunia ya kitani (sacks and bags of jute or other textile bast fibers of heading 53.03) yanayotambulika kwa HS Code 6305.10.00 yanayoagizwa kutoka nje. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vya ndani vinavyotengeneza magunia ya katani, kukuza na kuendeleza kilimo cha zao la mkonge hapa nchini pamoja na kuongeza ajira na mapato ya Serikali;
(h) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 0 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye unga wa kakao unaoingizwa kutoka nje unaotambulika kwa HS Code 1805.00.00. Lengo ni kuchochea na kuhamasisha kilimo cha zao la kakao nchini pamoja na kuongeza mapato ya Serikali;
(i) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya kuhifadhia kahawa vinavyotumiwa na viwanda vya kusaga kahawa nchini. Vifungashio vitakavyohusika ni vile vinavyotambulika katika HS codes 7310.21.00; 6305.10.00; 3923.50.10; 3923.50.90 na 3920.30.90. Hatua hii inalenga kuongeza thamani kwenye zao la kahawa na kuvipa unafuu wa gharama viwanda vinavyosaga kahawa hapa nchini. Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika katika kuagiza vifungashio hivyo;
(j) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya kuhifadhia korosho. Vifungashio vitakavyohusika ni vile
vinavyotambulika katika HS code 3923.21.00. Hatua hii inalenga kuongeza thamani kwenye zao la korosho na kuvipa unafuu wa gharama viwanda vinavyochakata korosho hapa nchini. Aidha utaratibu wa “Duty Remission” utatumika katika kuagiza vifungashio hivyo;
(k) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya kuhifadhia pamba. Vifungashio vitakavyohusika ni vile vinavyotambulika katika HS codes 3920.30.90; 6305.39.00 na 7217.90.00. Hatua hii inalenga kuvutia uwekezaji ili kuongeza thamani ya zao la pamba nchini;
(l) Kupunguza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 kwenye malighafi za kutengeneza taulo za watoto (Baby Diapers) zinazotumbulika kwa HS code 3506.91.00 Hot Melt Adhesive; PE film HS Code 3920.10.90, Empty bag for Baby Diapers HS Code 6305.33.00, Plastic cask HS Code 3926.90.90; na kiwango cha awali cha asilimia 10 kwenye Super Absorbent Polymer HS Code 3906.90.00, Wet strength paper HS Code 4803.00.00, Non-woven HS Code 5603.11.00, Polyethylene laminated Nonwovens HS Code 5903.90.00, Spandex HS Code 5402.44.00 na Dust free paper HS Code 4803.00.00. Aidha, msamaha huu utatolewa kwa utaratibu wa “Duty Remission”. Hatua hii inatarajiwa kutoa unafuu wa gharama za uzalishaji na kuongeza ajira;
(m) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 kwenye vifaa vinavyotumika katika kukata, kung’arisha na kuongeza thamani ya madini ya vito vinavyotambulika kwa HS Codes 6804.10.00; 7018.90.00;
7020.00.99; na kiwango cha awali cha asilimia 10 kwenye HS Codes 3606.90.00; 6813.20.00; 8202.20.00; 8202.99.00; 8203.20.00; 8205.10.00; 8423.89.90; 8513.10.90; na 9002.19.00. Hatua hii inalenga kuchochea uongezaji wa thamani kwenye madini. Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika katika kuagiza vifaa hivyo;
(n) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 kwenye makaratasi (HS Code 4805.24.00 na 4805.25.00) yanayotumika kama malighafi ya kutengeneza vifungashio aina ya maboksi (corrugated boxes). Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika. Lengo la hatua hii ni kuwapa unafuu wazalishaji wa vifungashio hivyo hapa nchini ili wananchi waweze kuvipata kwa bei nafuu;
(o) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 kwenye vifungashio vya mbegu vinavyotambulika katika HS codes 3923.29.00; 6305.10.00; 4819.40.00; 7310.29.90; 6305.33.00; 6305.20.00; 6304.91.90 na 7607.19.90. Utaratibu utakaotumika kutoa unafuu huo ni wa “duty remission”. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa mbegu hapa nchini;
(p) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye kahawa inayotambulika kwa Heading 09.01 inayoagizwa kutoka nje ya nchi. Lengo la pendekezo hili ni kulinda viwanda vya ndani na kuhamasisha kilimo cha kahawa hapa nchini
pamoja na kuongeza ajira katika sekta ya kilimo;
(q) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 au dola za kimarekani 125 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwenye bidhaa za chuma kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa. Bidhaa hizo ni “Flat – rolled products of iron or Non-alloy steel na Flat –rolled products of other alloy steel.” Bidhaa hizi hutambulika katika HS Codes 7209.16.00; 7209.17.00; 7209.18.00; 7209.26.00; 7209.27.00; 7209.28.00; 7209.90.00;
7211.23.00; 7211.90.00; 7225.50.0 na 7226.92.00. Lengo la kuendelea kutoza viwango hivyo ni kulinda viwanda vya hapa nchini, kukuza ajira pamoja na kudhibiti udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa hizo kutoka nje;
(r) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo (metric ton) kwenye bidhaa za mabati zinazotambulika kwa HS codes 7210.41.00; 7210.49.00; 7210.61.00; 7210.69.00; 7210.70.00 na 7210.90.00 kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa badala ya ushuru wa asilimia 25 au dola za kimarekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo
(metric ton), kwa mwaka mmoja. Lengo la hatua hii ni kuwalinda wazalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini kutokana na ushindani wa nje;
(s) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 au dola za kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwenye bidhaa za mabati zinazotambulika katika HS Code 7212.60.00 badala ya ushuru wa asilimia 10 pekee. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vya ndani kutokana na udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa hizo zinapoingizwa kutoka nje (under-invoicing and under valuation), na kulinda ajira na mapato ya Serikali;
(t) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwenye bidhaa za mabati kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa. Ushuru huo unahusu bidhaa zinazotambulika katika HS Code 7212.30.00; 7212.40.00 na 7212.50,00. Hatua hii ina lengo la kulinda viwanda vya ndani kutokana na udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa hizo zinapoingizwa kutoka nje (under invoicing and under valuation), na kulinda ajira na mapato ya Serikali;
(u) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za kimarekani 250 badala ya kiwango cha asilimia 25 au dola za kimarekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo (metric ton) kwenye bidhaa za chuma kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwenye nondo kwa mwaka mmoja. (Reinforment bars and hallow profile). Hatua hii inahusu bidhaa zinazotambulika katika HS codes 7213.10.00; 7213.20.00; 7213.99.00; 7214.10.00; 7214.20.00; 7214.30.00; 7214.90.00; 7214.99.00; 7215.10.00; 7215.50.00; 7215.90.00; 7225.90.00; 7225.92.00; 7225.99.00; 7306.30.00; 7306.50.00; 7306.61.00; 7306.69.00; na 7306.90.00. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vinavyozalisha nondo hapa nchini na kuongeza ajira;
(v) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za mboga mboga (horticultural products) zinazotambulika kwa HS codes 0603.11.00; 0603.12.00; 0603.13.00; 0603.14.00; 0603.15.00; 0603.19.00; 0604.20.00; 0604.90.00; 0701.90.00; 0702.00.00; 0703.10.00; 0703.20.00; 0703.90.00; 0706.10.00; 0706.90.00; 0710.10.00; 0710.21.00; 0710.22.00; 0710.30.00; 0714.10.00; 0714.20.00; 0804.30.00; 0804.40.00; 0804.50.00;
0805.10.00; 0805.40.00; 0805.50.00; 0806.10.00; 0807.11.00; 0807.20.00; 0808.10.00; 0808.30.00; 0910.11.00 na 0910.12.00. Lengo la hatua hii ni kulinda wakulima wa ndani ili kuendeleza kilimo cha matunda, mbogamboga na maua hapa nchini;
(w) Kutoza ushuru wa forodha kwa kiwango cha asilimia 10 badala ya asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za fito za plastiki zijulikanazo kama PVC Profiles HS Code 3916.10.00; 3916.20.00; 3916.90.00 ambazo hutumika kwa ajili ya kutengenezea fremu za milango, madirisha n.k. Lengo la hatua hii ni kuongeza mapato ya Serikali;
(x) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye karatasi zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini ambazo zinazotambulika kwa HS codes 4804.11.00; 4804.21.00; 4804.29.00; 4804.31.00 na 4804.41.00. Lengo la hatua hii ni kuendelea kulinda viwanda vinavyozalisha karatasi hizo hapa nchini;
(y) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 35 kwenye ngano inayotambulika kwa HS Code 1001.99.10 na HS Code 1001.99.90 kwa utaratibu wa “Duty Remission” ambapo wanaonufaika na unafuu huu ni wenye viwanda vya kusaga ngano. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama kwa Viwanda vinavyozalisha unga wa
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.