WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni imara na ina nia ya dhati ya kuendelea kuwatumikia watanzania kwa kufikisha maendeleo kwenye sekta zote za huduma za jamii katika kila eneo nchini
Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatatu Februari 26, 2024) alipozungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa maeneo ya Mariwanda na Sabasita wakati wa ziara ya kikazi Bunda mkoani Mara.
“Serikali ya awamu ya sita inawapenda watanzania wote ndio maana Rais wetu Dkt. Samia anatekeleza miradi mbalimbali ya maeneo katika sekta zote za maendeleo kuanzia ngazi ya Taifa hadi vijijini”
Akizungumza baada ya kukagua mradi wa shule ya msingi sabasita, Mheshimiwa Majaliwa amesema ni mkakati wa Serikali ya awamu ya sita kujenga shule kwenye kila kijiji na vitongoji vikubwa, kama kuna kijiji kina watu wengi mpango ni kuongeza shule
Ameongeza kuwa Sekta ya mifugo ni maisha na ni uchumi ndio maana Serikali Serikali imeanza na inaendelea na uratibu wa mpango wa kuwa na viwanda vya mazao ya mifugo “endeleeni kufuga na mzingatie masharti ya ufugaji ili muweze kukuza uchumi wenu”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.