SHIRIKA la Reli Tanzania - TRC limeendelea na mchakato wa ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kama Wataalam wa shirika hilo walipokutwa (pichani) wakiendelea na kazi ya kuweka kokoto juu ya tuta la reli ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuweka mataruma na kuanza kutandika reli ya kisasa - SGR hivi karibuni jijini Dodoma.
Mradi huu wa reli ya kisasa (SGR) nchini unalenga kuleta maendeleo ya watu kwa kurahisisha usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo hatua itakayopunguza muda mwingi unaopotea barabarani na kuwafanya wananchi kuwahi kufanyakazi nyingine za maendeleo.
Ujenzi wa mradi unaendelea ambapo kipande cha Morogoro hadi Mkutupora, Singida kina jumla ya kilomita 422 ambapo kilomita 336 zinajumuisha njia kuu na kilomita 86 ni sehemu za kupishania treni.
Chanzo: tzrailway (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.