Na. Dennis Gondwe, DODOMA
KATA ya Hombolo Makulu imetakiwa kujipanga kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika tarehe 23 Agosti, 2022 ili wananchi wote waweze kuhesabiwa na kuiwezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri alipokuwa akiongea na wananchi wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma ilipotembelea na kukagua hali ya ujenzi wa shule ya sekondari Hombolo Makulu.
Shekimweri alisema “Mheshimiwa Diwani, tutakapokuja hapa tutakuja kwa ajili ya mkutano mkubwa. Ila tarehe 23 Agosti, 2022 tuna Agenda ya Sensa ya Watu na Makazi. Nikuombe kwa nafasi yako kama Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ngazi ya kata pamoja na timu yako muendelee kusukuma hamasa ya timu yako kujitokeza kuhesabiwa na kusiwe na kisingizio kwenye siku hizo. Na kwenye Agenda hiyo, tuhimize pia makundi maalum hususani watu wenye ulemavu. Mara nyingi huwa tunawaacha nyuma kwa hiyo, tukuombe Diwani kuhamasisha na sisi tutakuja kukuongezea nguvu”.
Alisema kuwa ni muhimu kwa watu wote kuhesabiwa siku ya Sensa. Takwimu sahihi ya watu itaiwezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi wake. Taarifa na mipango hiyo inaisaidia serikali kupanga vipaombele vyake, alisema.
Kwa upande wake Juma Msumi alisema kuwa amekuwa akiisikia elimu ya Sensa ya Watu na Makazi katika vyombo vya Habari. Alisema kuwa Sensa ni muhimu kama ilivyo mipango mingine ya serikali na kuwashauri watu wote kujitokeza kuhesabiwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.