OR-TAMISEMI
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, amewataka maafisa tarafa na watendaji wa kata kuzingatia maadili nauwajibikaji katika utumishi wa umma.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Alhaj Shekimweri amesema serikali inatarajia kuona tija, umahiri na nidhamu ya hali ya juu kwa watumishi hao, hasa katika kusimamia mapato na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Baada ya mafunzo haya, tunatarajia kuona mabadiliko chanya. Ninyi ni kiunganishi muhimu kati ya serikali na wananchi, hivyo hakikisheni mnakuwa wasikivu, mnatatua kero za wananchi kwa haraka na kuimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo yenu,” amesema Shekimweri.
Amesisitiza pia usimamizi madhubuti wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana, hususan kwenye miradi inayotekelezwa kwa kutumia mfumo wa force akaunti unaohusisha mafundi wazawa.
Mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa kwa waajiriwa wapya katika mwaka wa fedha 2024/2025, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi mkubwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.