Na. Coletha Charles, Dodoma
Katibu Mkuu wa Shirika la Kutetea Haki za Abiria nchini (SHIKUHA), Mhandisi Hashim Ramadhani, amewataka abiria kuelewa elimu na haki zao wanapotumia huduma za usafiri kwa kushirikiana na Afisa Usalama barabarani ili kuhakikisha mabasi yanazingatia sheria na huduma bora.
Akizungumza katika mkutano na wajumbe wa shirika hilo kutoka mikoa mbalimbali katika ukumbi wa mikutano wa Rafiki Hoteli jijini Dodoma, Katibu Mkuu alifafanua kampeni za elimu zimekuwa muhimu katika kuhakikisha abiria wanakuwa na uelewa wa kina kuhusu haki zao.
Alisema kuwa, elimu hiyo inatolewa kupitia stendi za mabasi, masoko na sehemu zenye mikusanyiko. Pia alibainisha kuwa maafisa wa shirika hilo watashirikiana na wadau wa sekta ya usafiri kuhakikisha sheria na kanuni zinatekelezwa kwa maslahi ya abiria. “Tumeweka msisitizo katika kuwaelimisha abiria juu ya jinsi ya kuripoti changamoto wanazokumbana nazo, kama vile kucheleweshwa kwa safari, kupotea kwa mizigo, au huduma zisizokidhi viwango na tutashirikiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na Polisi. Lengo letu ni kujenga mazingira ya usafiri yenye uwazi, haki, na heshima kwa abiria,” alisema Ramadhani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Abiria nchini Kanda ya Kati, Anord Kisukuli, alisema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa abiria ili kuhakikisha huduma za usafiri zinakuwa salama, zenye ubora, na zinazingatia haki za kila mtumiaji. “Abiria wengi hawawezi kutoa taarifa Polisi wanakuwa wanahofu. Sisi kama SHIKUHA tunachanzo cha kupokea taarifa kama kupiga simu na vyanzo vingine. Hivyo, tunawasihi wapige simu waseme na tunazifikisha kwa mamlaka husika. Kwahiyo, abiria wasiwafumbie macho madereva wanaopenda kuendesha magari wendo ambao hauruhusiwi hadi matokeo yake wanasababisha ajari na watu wanapoteza uhai na viungo” alisema Kisukuli.
Nae, Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Abiria nchini Kanda ya Kusini, Mwalami Shaweji, alibainisha kuwa viongozi wamepewa barua za udhibiti wa kuwapa abiria elimu ya kujua haki zao. “Niwajibu wetu sasa kama viongozi kuwapa elimu abiria na kuwafahamisha kuhusu haki zao, tunajukumu nchi nzima na tunaomba sana ushirikiano kwa sababu wao ndiyo walengwa wasiwe waoga kutoa taarifa. Lakini pia niiombe serikali pindi tunapotoa taarifa zifanyiwe kazi kwa haraka” alisema Shaweji.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.