WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt, Doroth Gwajima amesema mashindano ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesaidia kuitangaza Tanzania duniani
Gwajima ametoa kauli hiyo kwenye mashindano ya Dunia ya urembo, utanashati na mitindo linalofanyika jijini Dar es Salaam wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu Hassan.
Amempongeza Mhe. Rais kwa kutoa kipaumbele kwenye michezo na kusisitiza kuwa mashindano haya ya michezo na utamaduni yanasaidia kuleta upendo, mshikamano na udugu kwa mataifa mbalimbali.
Amewasihi wazazi wenye watoto walemavu kuwatoa watoto wapate elimu ili waweze kuonyesha vipaji vyao badala ya kuendelea kuwaficha majumbani na kuongeza kuwa sera ya utamaduni 1997 inaeleza ushiriki wa watu wenye ulemavu kwenye utamaduni."Hii imetuonesha kuwa sisi sote ni sawa mbele za Mungu mimi naweza kuwa sina hiki na wewe ukawa na hiki" ameongeza Gwajima
Amesema kupitia mashindano haya na onyesho la Filamu ya Royal tour waliyoitazama watakuwa mabalozi wazuri wa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo anayotoa kwenye sekta anazoziongoza ambapo kutokana na maelekezo hayo kumekuwa na mafanikio makubwa.
Amefafanua kuwa wizara yake itaendelea kutafsiri na kutekeleza kikamilifu maelekezo yote yanayotolewa na Rais na Serikali kwa ujumla.
Aidha amesema jukumu la Wizara yake ni kuleta furaha na Faraja kwa watanzania na kwamba shindano hili ni mwendelezo wa Royal Tour.
Mchengerwa ametoa zawadi ya kinyago kwa Rais wa Dunia wa Mashindano hayo Bonita Lee.
Shindano hili limepambwa na wasanii mbalimbali waliotumbuiza na kuwafanya watazamaji kupata burudani ya kutosha.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.