Na Mwalimu Malick Masoud, Dodoma
MASHINDANO makubwa ya kitaaluma yanayohusisha shule za sekondari za jiji la Dodoma yanayojulikana kama ‘Dodoma Inter School Debate Competition’ ambayo yapo chini ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri yanaendelea katika Shule ya Sekondari Dodoma.
Mashindano haya ya mdahalo kwa wanafunzi yameasisiswa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri yakiwa na lengo la kuwajengea wanafunzi uwezo na ari ya kujiamini, kujieleza, kujenga hoja, kuhoji na zaidi kuwajengea uwezo wa maarifa na kitaaluma. Wakati mashindano haya yakiendelea, yameibua matumaini mapya ya ari kwa wanafunzi kufanya vema katika masomo na maisha kwa ujumla.
Mdahalo huu una mada zinazohusu upingaji wa ukatili wa kijinsia kwa lugha ya kingereza na kiswahili.
Ofisi ya Mkuu wa wilaya imeanzisha mashindano kwa lengo la kuinua ufaulu kwa wanafunzi yakihusisha shule takribani 16, kati ya shule hizo ni Dodoma Sekondari, Viwandani, Umonga, Kisasa, Hazina, Sechelela, Nzuguni, Kiwanja cha Ndege, Mnadani, Mkonze, Mlimwa, Miyuji, Chinangali na shule ya Kizota zilizoshiriki huku shule ya Kikuyu na Makole hazikufika kushiriki.
Katika mashindano hayo ambayo yamekuwa na mchuano mkali na wa kuvutia kwa vijana kutokana walivyoweza kujibizana kwa hoja na kutetea hoja na maswali mbalimbali yaliyoulizwa yamewezesha shule kama Dodoma sekondari, Nzuguni, Sechelela, Miyuji, Mnadani, Mkonze na Kiwanja cha ndege kuweza kufuzu hatua inayofuata huku shule ya sekondari Kisasa ikifanikiwa kuingia kama ‘Best Looser’ kwa hatua ya nusu fainali inayoendelea.
Mashindano haya yalizinduliwa na Afisa Tarafa Wa Dodoma Mjini Bi. Zainabu Issa ambaye alimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini.
Akitoa salamu za wakuu wa shule na kwa niaba ya Afisa Elimu Sekondari Mwenyekiti wa TAHOSA Mwalimu Fred Nyandoro alisema wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, pia kwa Kamati nzima ya maandalizi ya mashindano haya kwa kuhakikisha kila jambo jema linalohusu elimu linafanikiwa na kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi na Walimu kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Shindano hili Mwalimu Malick Masoud aliitambulisha kamati yenye wajumbe ambao ni Mwalimu Yasin Mponda, Mwalimu Ester Bahati, Salimu Dewji, Christina Mwinuka, Nurdin Ngapanya na Mwalimu Kasimu Njonjoro. Mwenyekiti Masoud aliwashukuru sana waratibu wote waliosaidiana katika jambo hili kubwa na kuwaomba kuendelea kushirikiana kwa kila hatua.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.