Shirika la John Snow Incorporation (JSI) kwa kushirikiana na World Education Inc, chini ya makubaliano kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Marekani kupitia msaada wa watu wa Marekani USAID, lilianza kufanya kazi Mkoani Dodoma mwaka 2014 likitekeleza mradi wa kuimarisha mifumo ya utoaji huduma za afya na Ustawi wa Jamii katika Halmashauri 84 Tanzania ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
Katika kutekeleza mradi huu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Idara ya Ustawi wa Jamii na TAMISEMI iliandaa mfumo jumuishi wa kitaifa wa usimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii. Mafunzo hayo yalifanyika hapa Mkoani Dodoma mwanzoni mwa mwezi August 2017 kwa wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii (CCW). Mafunzo haya yalijumuisha wasimamizi wa mashauri ya watoto wapatao 144 wakiwemo (wanawake 78 na wanaume 66) kutoka katika Kata 30 za Manispaa ya Dodoma pamoja na wasimamizi wao 22 wakiwemo yaani wanawake 14 na wanaume 8). Jumla ya wasimamizi wote waliopata mafunzo ni 66 kwa Manispaa ya Dodoma.
Kufuatia mafunzo hayo Shirika la John Snow Incorporation pia limewapatia wasimamizi wa wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii vitendea kazi ambavyo ni baiskeli na makabati ya kuhifadhia vyaraka. Zoezi hili la kukabidhi vitendea kazi hivyo lilifanyika leo tarehe 17.01.2018 katika ngazi ya Halmashauri likimhusisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma Mh. Profesa Davis Mwamfupe na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma ndugu Godwin Kunambi, Afisa Ustawi wa Jamii Beatrice Lyimo na wasimamizi wa wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya Kata kutoka katika Kata 25 za Manispaa ya Dodoma.
Shirika la John Snow Incorporation (JSI) limetoa vitendea kazi hivyo, baiskeli 25 ili kurahisisha usafiri katika maeneo yao mbalimbali ya kazi na makabati 16 kwa ajili ya kuhifadhi taarifa mbalimbali za utendaji wa kazi zao za kila siku. Shirika lilikabidhi vitendea kazi hivi kwa Mstahiki Meya na Mkurugenzi ambao walifanya jukumu la kukabidhi rasmi vitendea kazi hivyo kwa wasimamizi wa wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya Kata.
Kata zilizopatiwa vitendea kazi hivyo ni kata ya Kilimani. Viwandani, Dodoma Makulu, Chigongwe, Chamwino, Nkuhungu, Kizota, Ipagala, Makole, Nala, Tambukareli, Kikuyu Kaskazini, Kikuyu Kusini, Iyumbu, Ipala, Mpunguzi, Mbabala, Mkonze, Matumbulu, Kiwanja cha ndege, Miyuji, Nghong`onah, Hazina, Madukani na Ntyuka.
Kutazama picha zaidi za tukio hili, Bofya hapa:
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.