WAGANGA Wakuu wa Halmashauri nchini wametakiwa kushirikiana kwa karibu na Wakurugenzi wao ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi.
Agizo hilo limetolewa Jijini Mbeya na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Charles Mahera wakati akizungumza na watumishi wa sekta ya afya wa mkoa huo.
Dkt. Mahera amesema kuwa watendaji hao wakishirikiana katika kutekeleza majukumu yao wataleta ufanisi katika kutoa Huduma bora kwa mwananchi.
“Natoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani mpaka sasa ametoa kiasi cha shilingi Bilioni 900 kwa ajili ya sekta ya afya”, ameeleza Dkt. Mahera
Alisema kuwa uwekezaji wa wataalamu, ujenzi wa miundombinu, vifaa na vifaa tiba, nyumba za watumishi, dawa na vitendanishi lengo ni wananchi kupata Huduma bora hivyo ni wajibu watendaji hao kushirikiana ili kuweza kufikia malengo.
Aidha, amewataka makatibu wa afya katika vituo vya kutolea Huduma za afya kufanya majukumu yao kwa ufasaha ili kuleta matokeo katika nafasi zao.
“RCHMT na CHMT fanyeni tekelezeni majukumu yenu ili kuleta ubora wa Huduma katika vituo vya kutolea Huduma na lazima mlete matokeo chanya yatakayo mgusa mwananchi moja kwa moja”, ameelekeza Dkt. Mahera
Vile vile amewataka kuhakikisha wanashirikisha jamii katika vijiji na kata ili kujua nini kinafanyika katika maeneo yao na kuwapa nafsa wananchi kushiriki katika maendeleo mbalimbali katika maeneo yao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.