MADIWANI wa Viti maalumu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametembelea na kukagua ujenzi wa shule ya mfano ya Msingi inayojengwa Kata ya Ipagala Jijini humo.
Shule hiyo inayotarajiwa kufunguliwa mwezi Machi mwaka huu inajulikana kwa jina la Mtemi Mazengo Shule ya Msingi na itachukua wanafunzi kutoka maeneo ya jirani na Kata hiyo.
Mkuu wa Shule ya Msingi Ipagala B ambaye anasimamia ujenzi katika shule hiyo Imani Weston amesema hadi sasa ujenzi katika shule hiyo umefikia asilimia 95 ambapo kazi iliyobaki ni kukamilisha ujenzi wa chemba za vyoo.
“Shule hii itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 705 tunatarajia itaanza kazi baada ya likizo ndogo ya mwezi Machi mwaka huu” alisema Mwalimu Weston.
Alisema wanafunzi hao watatoka katika shule za Chadulu, Medeli , Mlimwa C, Ipagala na Ipagala B ambazo zote zipo jirani na shule hiyo, na kwamba kigezo cha uwezo wa mwanafunzi kitazingatiwa ili asajiliwe.
“Shule hiyo ina madarasa 17, vyoo vya wanafunzi jinsia zote na walimu, nyumba za walimu, bwalo la chakula, viwanja vya michezo, maabara na maktaba, tunaishukuru sana Serikali kwa mradi huu muhimu” alisema Weston.
Wakizungumza wakati wa ziara hiyo, baadhi ya Madiwani hao walishauri shule hiyo iwe na mabweni ili kuwawezesha wanafunzi wa maeneo ya mbali na Kata ya Ipagala kupata fursa ya kusajiliwa na kusoma kwa kuzingatia uwezo wa mwanafunzi husika.
“Natamani sana shule hii iwe ya bwebi kwani wanafunzi wanaosoma katika shule hii watakuwa wanasajiliwa kwa kutazama uwezo wao darasani hivyo hawaishi hapa Ipagala wote, wapo watakaotoka shule za pembezoni, kama kutakuwepo na mabwebi kutawasaisdia sana watoto kutotembea kwa umbali mrefu kuja shuleni.
Jumla ya walimu 20 kutoka shule tano zitakazotoa wanafunzi watahamia na kufundisha katika shule hiyo ambayo inatarajiwa kuwa ya mfano kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma na ujenzi wake unagharamiwa na Serikali Kuu kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.