Kichaa cha mbwa (Rabies) ni ugonjwa unaowapata wanyama wote wanyonyeshao (Mbwa, Paka, Binadamu, Ng’ombe, nk)
Ugonjwa huu unasababishwa na kirusi (Rabies Virus), Virusi hawa wanashambulia mfumo wa fahamu.
Unavyoenea: Ugonjwa huu Huenea kwa njia ya mate.
Mate haya yanakua na virusi na yanaweza kumfikia mnyama mwingine kwa njia ya kuuma au kumtemea mate kwenye maeneo yenye vidonda, machoni, puani au mdomoni.
Virusi Husafiri toka sehemu waliyoingilia/iliyong’atwa na kwenda mpaka kwenye Ubongo kisha huzaliana na kurudi tena kwenye tezi za Mate (Mdomoni).
Dalili za ugonjwa huu hujitokeza kati ya siku 14 - 80 tangu mtu/mnyama apate maambukizi.
Dalili za Kichaa cha mbwa kwa binadamu
Ni muhimu kupata chanjo mara tu unapong'atwa na Mbwa kabla dalili kuonekana kwani ugonjwa huu hauna tiba
Dalili za Kichaa cha mbwa kwa wanyama
Uonapo mnyama mwenye mojawapo ya dalili hizi, toa taarifa haraka kwa Mtaalam wa Mifugo, Serikali ya Kijiji/Mtaa au Kata ili mnyama husika adhibitiwe
Jinsi ya kuhudumia jeraha lilitokana na kung'atwa na mnyama
Endapo mtu atang'atwa na Mbwa au mnyama mwingine aoshe jeraha kwa maji mengi yanayotiririka kwa angalau dakika 15. Kidonda kisifungwe, kisha apelekwe haraka kwenye kituo cha huduma za afya kupatiwa chanjo kuzuia madhara dhidi ya Kichaa cha Mbwa.
Mbwa na Paka wapelekwe kuchanjwa dhidi ya Kichaa cha Mbwa kila mwaka au kulingana na ushauri wa Mtaalam wa Mifugo.
KUMBUKA: Chanjo ni njia pekee inayotumiaka kumkinga Mbwa na wanyama wengine dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Kichaa cha Mbwa.
SAMBAZA UJUMBE HUU, OKOA MAISHA
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.