Taasisi ya DOYODO kwa kushirikiana na shirika la MULIK-Tanzania, YUNA-Tanzania na The Green Icon wameadhimisha siku ya mabadiliko ya Tabia ya Nchi jijini Dodoma.
Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye aliwakilishwa na mkuu wa wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius Ndejembi.
Maadhimisho haya yalianza kwa maandamano kutokea Viwanja vya Bunge la Tanzania jijini Dodoma hadi kwenye eneo la Nyerere Square. Maandamano haya yalishirikisha Watendaji wa Kata, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, wanavyuo na wananchi mbalimbali waliojitokeza.
Aidha, katika hotuba yake, Mhe. Ndejembi alihimiza kuundwa club za mazingira mashuleni zitakazo kabiliana na Mabadiliko ya TabiaNchi kwa kutoa elimu na kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo.
Vile vile Mkurugenzi Mtendaji wa DOYODO Rajabu Juma Suleiman alisisitiza kuwa ni jukumu letu sote kuhakikisha tunatatua athari zinazosababishwa na mabadiliko ya TabiaNchi, Suleiman aliishukuru Serikali kwa jinsi inavyoendelea kuiamini taasisi ya DOYODO na kuzidi kushirikiana katika kusukuma mbele gurudumu ya maendeleo ya nchi yetu hususani kwa kutumia na kuwaandaa vijana.
Baadhi ya picha za matukio mbalimbali yaliyojiri wakati wa maadhimisho.
Mwakilishi wa mgeni rasmi Mhe. Deogratias Ndejembi Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akiteta jambo na mmoja wa waandaaji wa maadhimisho ya Siku ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya DOYODO Rajabu Juma Suleiman.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Dodoma Sharifa Nabalang'anya akiongea wakati wa maadhimisho hayo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.