Dondoo kuhusu moyo
Watu milioni 17.9 duniani wanafariki kila mwaka kutokana na magonjwa ya moyo.
Watu wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo wanashauriwa kutumia dawa kama walivyopangiwa na watoa huduma za afya.
Magonjwa ya moyo yanaweza yasioneshe dalili yoyote mapema hivyo ni muhimu kupima afya yako mara kwa mara ili kupata tiba mapema.
Dhamilia kulinda afya ya moyo wako kwa:
• Kupima afya
• Kufanya mazoezi
• Ulaji unaofaa
• Kuepuka sigara
Linda afya ya moyo wako:
• Fanya mazoezi angalau mara 3 kwawiki, kwa muda wa dakika 30
• Usivute sigara au kutumia bidhaa yoyote ya tumbaku
• Punguza vyakula vyenye mafuta, sukari na chumvi kwa wingi
• Usinywe pombe kupita kiasi
• Epuka uzito mkubwa kupita kiasi, unene au kitambi
• Fanya uchunguzi wa afya yako mara kwa mara
Linda afya ya moyo wako, kula matunda na mbogamboga katika kila mlo
Magonjwa ya moyo yanaongoza kwa kusababisha vifo vingi duniani
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.