Na WMJJWM, Dar Es Salaam
Kuelekea maadhimisho ya Siku ya mtoto wa kike Mamlaka za Serikali za Mitaa zimeshauriwa kuhakikisha hamasa inatolewa kwa watoto wa kike kushiriki katika uchaguzi kwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye majukwaa yao katika ngazi za shule na kwenye jamii.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju ametoa rai hiyo Oktoba 02, 2024 jijini Dar Ea Salaam wakati akizungumza na waandishi wa Habari.
Mpanju amebainisha kwamba, Serikali inaratibu uanzishwaji wa majukwaa mahsusi kwa ajili ya kuwajengea uwezo watoto shuleni kwa usaidizi wa walimu wa malezi na unasihi ili kukabiliana na ukatili unaoweza kutokea nyumbani, barabarani na shuleni, ambapo kufikia Septemba, 2024 jumla ya madawati 3,618 yameundwa, kati ya hayo 2,471 katika shule za msingi na 1,147 katika shule za sekondari.
Amesema, Kaulimbiu ya maadhimisho kwa mwaka huu ni “Mtoto wa Kike na Uongozi; Tumshirikishe, Wakati ni Sasa” ambayo, inahimiza uhamasishwaji wa mtoto wa kike kushiriki katika kugombea nafasi za uongozi kwenye chaguzi zote kwa umri wake ili ajifunze na apate stadi za uongozi kwa lengo la kumuandaa kuwa kiongozi wa sasa na siku za baadaye.
“Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi za mwaka 2022, idadi ya watoto kwa Tanzania Bara ni milioni 29,365,234 ambapo kati yao watoto wa kike ni milioni 14,680,895 sawa na nusu ya watoto wote nchini. Kundi hili hili la watoto wa kike linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitendo vya ubakaji, ulawiti, mimba na ndoa za utotoni.” amesema Mpanju.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.