Siku ya Usafi Duniani (World Cleanup Day) kwa mwaka 2020 leo tarehe 19 Septemba imeadhimiwa Jijini Dodoma kwa shughuli za usafi kama ilivyo ada katika viunga vya Jiji la Dodoma kufanya usafi kwenye maeneo ya makazi na sehemu za biashara kwa umbali wa mita tano.
SIKU hii ya kimataifa ambayo huadhimishwa kila mwaka ikiwa na lengo la kuiepusha dunia na matatizo yanayosababishwa na uchafu, ikiwemo uchafu wa baharini, huadhimishwa kwa watu kukusanya uchafu pamoja na kufagia, kazi ambazo hufanyika karibia kila mwaka kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.
Jiji la Dodoma lilifanya usafi katika Mto Pombe unaopita katika kata za Madukani, Majengo na Uhuru ambao uliwashirikisha pia kampuni ya Green Waste, taasisi ya usafi ikulikanayo kama 'Nipe Fagio', vikundi vya usafi na wanafunzi wa shule ya Sekondari Viwandani.
Akiongea baada ya shughuli ya usafi kukamilika, Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu Dickson Kimaro aliwataka pia wamiliki wa mabasi kuhakikisha kila basi linakuwa na chombo cha kuhifadhia taka ndani ya basi, na kutoa tahadhari kwa abilia kutotupa taka hovyo wanapokuwa ndani ya magari na wanapopita Jijini Dodoma, na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka utaratibu huo.
Naye Afisa Mazingira Ally Mfinanga aliwataka wananchi wa Dodoma kuufanya usafi kuwa tabia ili kuepukana na uchafu, kitu ambacho kitasaidia sana kuondoa magonjwa yanayosababishwa na uchafu kama vile kipindupindu, kuhara na kadharika, lakini pia Jiji la Dodoma kama Makao Makuu ya Nchi litazidi kuwa safi, salama, lenye kupendeza na mfano kwa miji na majiji mengine.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.