KATIKA mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali kupitia Wakara wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) ilitenga shilling milioni 622.52 kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa mita 45 na upana wa mita 7, ujenzi wa boksi, karavati kubwa katika mto Nangalu lenye urefu wa mita 26.8 na upana wa mita 9, kuchonga barabara yenye urefu wa kilometa 10.3 kuweka changarawe kilometa 2 na kuchimba mifereji ya kuondoa maji barabarani.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa David Sillinde leo Novemba 8, 2022 Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbuge wa Jimbo la Mchinga Salma Rashid Kikwete lililouliza kuwa Serikali inampango gani wa kujenga barabara ya Moka Mtumbikile hadi Matimba kwa kiwango cha Changarawe.
Sillinde amesema Serikali kupitia TARURA itajenga barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe kadri ya upatikanaji wa fedha baada ya kukamilisha ujenzi wa vikwazo vya barabara hiyo.
Aidha, Silinde amesema Serikali inamkakati wa kupandisha hadhi barabara za udongo kwenda changarawe na zile za changarawe kwenda kiwango cha lami na kufungua barabara nyingine mpya.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.