NAIBU Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amesema Wizara imedhamiria kuwawezesha vijana katika Sekta ya Kilimo kwa kuwapatia zana mbalimbali ikiwemo matrekta ili waweze kulima kwa tija.
Mhe. Silinde amesema hayo wakati akikabidhi matrekta tisa kwa wakulima kutoka Kampuni ya PASS Leasing Company Limited katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.
“Serikali imejipanga katika kuhakikisha Mikoa na Halmashauri zote nchini zinatenga maeneo ya shughuli za kilimo kwa ajili ya vijana ili Taifa letu la lijitosheleze na mazao ya kilimo,” amesema Naibu Waziri Silinde.
Aidha, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya PASS Leasing Limited, Rosebud Kurwijila amesema kampuni hiyo imekabidhi vifaa vya kulimia kwa wakulima zikiwemo trekta 9 zenye thamani millioni 401.76 kwa wakulima wa mkoa wa Dodoma, wilaya za Kongwa na Chemba.
“Uwezeshaji huu tunategemea utakwenda kuongeza uzalishaji kwa kulima mashamba zaidi ya ekari 2000; kutengeneza ajira za moja kwa moja zisizopungua 30 na kuwafikia wanufaika takribani 300 kwa kipindi cha msimu mmoja,” amesema Rosebud Kurwijila.
Wizara ya Kilimo imeendelea kuhamasisha matumizi ya zana bora za killmo ikiwa ni pamoja kujenga uwezo wa zana za kilimo na kuwawezesha wakulima kuwa na uhakika wa zana wanazotumia katika shughuli zao za kilimo ili kufikia dhamira ya Serikali kufikia matrekta 10,000 ifikapo mwaka 2030.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.