NAIBU katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Charles Mahera amewaelekeza wakurugenzi na watendaji katika Halmashauri kusimamia miradi ya maendeleo kwa ukaribu ikiwemo miradi ya Afya ili kuongeza ufanisi na ubora katika miradi hiyo na kukamilika kwa wakati.
Hayo yamesemwa kwaniaba yake na Mkurugenzi msaidizi wa Huduma za Ustawi wa jamii Bi. Subisya Kabuje katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma wakati akiongea na timu ya usimamizi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe wakati akihitimisha ziara ya siku mbili iliyofanyika Mkoani humo.
Amesema kumekuwa na huduma mbalimbali ambazo zinatolewa katika Halmashauri miongoni mwa hizo ikiwa ni huduma feet family kwa Watoto waliopoteza familia zao ambapo Maafisa Ustawi wa Jamii wanajukumu la kufatilia familia hizo na kujua changamoto zinazowakabili na kuzitatua.
Kwa upande wa miradi ya ujenzi amewataka wataalamu husika wa kushirikiana kwa ukaribu na wahandisi wa Mradi kwani wao ndio wanaelewa zaidi ni vitu gani vinahitajika katika Miradi hiyo.
“lakini pia hata kwenye miradi ambayo inahusika na maswala ya ujenzi wa vituo vya afya Mganga Mkuu wa Halmashauri hakikisha unafatilia kwa ukaribu ujenzi na sio kumuashia Mhandisi peke yake ili kuhakikisha majengo hayo yanakizi mahitaji maalumu yanayotakiwa.”
Pia amewaelekeza watoa huduma katika vituo vya Afya na Zahanati kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa pindi wanapokuja kupata huduma mbalimbali katika vituo hivyo kwani itasaidia kuwavutia zaidi wananchi na kuongeza mapato katika vituo vya Afya vya Serikali.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.