Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu kwa njia ya simu wakati wa Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Waandishi wa Habari ambapo amewataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi.
Tanzania imekua miongoni mwa nchi 50 Duniani, nchi ya 24 kwa Afrika na ya pili kwa Afrika Mashariki kuingia katika uchumi wa kati.
"Miaka mitano kabla ya lengo letu la Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 nchi yetu imeweza kuingia katika uchumi wa kati lakini hii haina maana tuache kuchapa kazi. Nawasihi Watanzania tuendelee kuchapa kazi.
Uchumi wa kipato cha kati ni ishara kuwa umasikini umepungua, uchumi imara unajengwa, uzalishaji viwandani unaimarika na wananchi wanapata maendeleo" amesema Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Tunampongeza Rais Magufuli na Serikali yake kwa kuweka rekodi ya tukio hili kutokea katika utawala wake, pia tunawashukuru na kuwapongeza Marais waliopita kwani wamefanya mengi yaliyochochea uchumi wakati wa utawala wao. Amesema Dkt. Abbas.
Uchumi wa kipato cha kati tulioingia tafsiri yake ni kuwa pato la mwananchi kwa mwaka ni USD 1,036 hadi USD 4,045.
Misingi kumi iliyotusaidia kuingia katika kipato cha kati ni amani na utulivu, mipango thabiti ya maendeleo, utekelezaji usioyumba, kufanya maamuzi magumu, azma ya kujitegemea, nidhamu katika matumizi.
Misingi mingine ni kuimarisha miiko ya uongozi, kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya kimkakati inayokuza uchumi, kuwekeza kwenye maendeleo ya watu pamoja na kujenga sekta binafsi yenye tija kwa maendeleo ya Taifa.
Chanzo: Idara ya Habari-Maelezo
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.