HALMASHAURI ya jiji la Dodoma imesema kuwa inatarajia kulivunja na kulijenga upya soko la Sabasaba ili kulifanya la kisasa zaidi na lenye hadhi ya Makao Makuu ya Nchi.
Mkurugenzi wa Jiji hilo Joseph Mafuru ametoa taarifa hiyo katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri hiyo lililokutana na Januari 26, 2022 katika ukumbi mkuu wa jiji.
Hatua hiyo imekuja kupitia mpango mkakati wa kuboresha mazingira katika jiji la Dodoma pamoja na kuboresha maeneo ya masoko na stendi kuu ya daladala ya jiji hilo iliyopo jirani na soko hilo.
“Tunatarajia ifikapo Julai mwaka huu tutaanza ujenzi wa soko la sabasaba na standi kupitia fedha za mradi wa Benki ya Dunia lakini kwa sasa tunamwaga kifusi katika stendi hiyo ili kuondoa adha kwa mabasi ya daladala na abiria kutokana na hali ya mvua katika wakati huu wa majira ya masika ”alisisitiza Mafuru.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa Soko la sabasaba linatakiwa kufumuliwa lote na kujengwa upya ili liwe na hadhi inayoendana na makao makuu ya nchi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.