MKANDARASI anayejenga miradi ya kimkakati ya Soko Kuu na Stendi Kuu ya kisasa ya mabasi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mohammedi builders kukamilisha na kukabidhi majengo hayo ifikapo tarehe 15 Februari, 2020.
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alipokuwa akiongea na wananchi wa Dodoma baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa majengo ya Soko Kuu na Stendi Kuu ya Mabasi ya Dodoma leo. Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza Soko Kuu jipya litakapokamilika liitwe kwa jina la Ndugai kwa heshima ya Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai.
Rais Dkt. Magufuli amesema “ifikapo tarehe 15 Februari, 2019 muwe mmekabidhi miradi hii”. Aidha, aliishukuru benki ya dunia kwa kuikopesha fedha Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo. “Shilingi bilioni 38 tumekopa, siyo za bure, tutazilipa kwa riba. Tumekopeshwa sababu tumeaminika na kuheshimika” alisisitiza Dkt. Magufuli.
Vilevile, aliutaka uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kumsimamia mkandarasi kukamilisha miradi hiyo kwa muda aliopangwa. “Fedha ya Serikali lazima itumike vizuri” alisisitiza Rais Dkt. Magufuli.
Wakati huohuo, amepongeza kwa kutengwa eneo kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo. “Bahati nzuri mmetenga eneo la machinga, wataingia na kufanya biashara zao na vitambulisho vya Machinga, hakuna kuwadai fedha” aliagiza Rais.
Mwonekano wa Soko Kuu la Dodoma lililopo eneo la Nzuguni ambalo limewekewa jiwe la msingi na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ujenzi wa Soko hili unatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2020.
Mwonekano kutoka angani wa Stendi Kuu ya mabasi ambayo ujenzi wake imewekewa jiwe la msingi na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Ujenzi huu unatarajiwa kukamilia mwezi Februari 2020
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.