SPIKA wa Bunge, Job Y. Ndugai (Mb), amezindua muungano wa wadau wa kupambana na kifua kikuu leo (tarehe 12 Septemba 2021) katika viwanja vya Nanenane Jijini Dodoma.
"Naipongeza kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na Kifua kikuu kwa jinsi wanavyoshughulika na baadhi ya mambo ambayo ni tatizo kubwa sana katika nchi yetu na kama ingeachwa kwa kamati ya huduma na maendeleo ya jamii pekee yasingeweza kuwa na mwanga wa kutosha" alisema Spika Ndugai.
Pia, aliwapongeza sana Wabunge vinara wa kupambana na kifua kikuu kwa ufuatiliaji wao wa karibu harakati za kifua kikuu na ukoma na kuhakikisha jitihada mbalimbali zinafanyika kutokomeza janga hili la ugonjwa wa kifua kikuu.
Aidha, aliwashukuru wadau wa maendeleo ambao wanashirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa TB.
Malengo na mipango ya kidunia na ya nchi yetu ni ifikapo 2025 TB iingie katika historia ya magonjwa yaliyowahi kuwepo hapa duniani.
Uzinduzi huo ulihudhuliwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwenyekiti kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Kifua kikuu, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wajumbe wa kamati pamoja na Wabunge vinara wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa TB.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.