Mradi wa TASAF III umeanza kutoa mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa Miradi ya kutoa ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (Local Service Provider - LSP).
Mafunzo haya yatafanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Mkoa wa Dodoma kuanzia tarehe 4 hadi 9 Septemba 2017, ambapo jumla ya Wasimamizi Wasaidizi 60 watapatiwa mafunzo.
Kwa mujibu wa mratibu wa TASAF katika Manispaa ya Dodoma Sekunda Kasese, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa wasimamizi wasaidizi hao kuhusu utekelezaji wa Miradi ya Ajira za Muda iliyoibuliwa na walengwa wenyewe katika Mitaa na Vijiji 73 vilivyo katika Mpango wa TASAF.
Kasese alisema kuwa, mafunzo hayo ya siku sita yanafadhiliwa na mradi wa TASAF Makao Makuu, na kwamba baada ya mafunzo, wasimamizi wasaidizi hao watarudi katika Vijiji na Mitaa yao kusimamia utekelezaji wa miradi kwa kipindi cha miezi minne, inayoanzia Septemba hadi Disemba mwaka huu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.