MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, leo Aprili 11, 2024 amefanya Mkutano na waandishi wa Habari (Press conference) kuhusu maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 102 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yatakayofanyika Aprili 13, 2024.
Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa ofisi yake jengo la Mkapa Jijini Dodoma lengo kuu la maadhimisho hayo likiwa ni kushirikisha Watanzania, Wizara, Taasisi n.k katika kumuenzi Baba wa Taifa kwa mazuri aliyotufanyia.
"Pamoja na maadhimisho haya, Tarehe 13/04/2024, Taasisi itakua na Mdahalo kuhusu umuhimu wa kudumusha Amani na mshikamano wa Taifa chini ya mwamvuli wa kauli mbiu isemayo 'Kudumusha Amani - ni haki na wajibu wetu kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu' pia, Taasisi itamuenzi Baba wa Taifa kwa kuasisi uhifadhi wa Maliasili za Taifa na Utunzaji wa Mazingira" Amesema Mhe. Senyamule
Kadhalika, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Taifa Ndugu Peter Mavunde ameeleza namna Taasisi yake inavyofanya kazi katika kuenzi mambo mbalimbali aliyoyafanya Baba wa Taifa.
"Taasisi hii ina miaka mitatu mpaka Sasa ambapo ilianza rasmi mwaka 2021 kwa kufanya Kongamano la miaka 100 ya kuzaliwa Baba wa Taifa. Mwaka 2022 walizindua Mpango wa kuwarithisha vijana wetu waliopo shuleni na vyuoni mambo mazuri aliyoyafanya Baba wa Taifa" Ndugu Peter Mavunde
Maadhimisho ya mwaka huu yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi za Kusini mwa Afrika, nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi rafiki, Viongozi wastaafu wa Kitaifa pamoja na viongozi wote wa ngazi tofauti tofauti za Serikali wakiwemo wanafunzi wa ngazi zote.
Maadhimisho ya mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopo Mtumba - Mji wa Serikali ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.