Na WMJJWM,Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju amewataka watekelezaji wa Mpango wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM)kuhakikisha wanatumia mipango na mbinu sahihi kutekeleza maazimio waliyojiwekea katika mkutano huo.
Mpanju ametoa maelekezo hayo wakati akifunga mkutano wa Kitaifa wa wadau hao uliofanyika kwa siku tatu kuanzia Desemba 11-13, Jijini Dodoma.
Amefafanua kuwa endapo wadau hao watatumia ipasavyo majukwaa ya kidini na Kiserikali kusambaza elimu kwa Wazazi, Walezi na Jamii kuhusu umuhimu wa kuwekeza kwenye Malezi na Makuzi ya Mtoto,kutakua na mabadiliko chanya yaliyokusudiwa.
“Kuwafikia viongozi wa dini ni suala la msingi kwani wao ndiyo wanaoshiriki kikamilifu katika hatua zote muhimu za mahusiano kabla ya mtoto kupatikana yaani, uchumba na ndoa, ni muhimu kuwekeza katika sekta hii ili kuhakikisha tunaowaandaa kuwa wazazi wanakuwa na elimu sahihi kuwajibika na kuwapatia watoto malezi chanya”amesema Mpanju.
Vilevile Mpanju amesema programu ya MMMAM imeshazinduliwa katika mikoa yote 26 na Halmashauri 70 kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali kwa ushirikiano wa Serikali, wadau wa maendeleo, Asasi za kiraia pamoja na Waandishi wa habari vinara ambao wamekua chachu kuhakisha mpango unatekelezwa katika ngazi zote.
Akizungumza na washiriki wa mkutano huo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Sebastian Kitiku amefafanua maazimio yaliyowekwa katika kikao hicho yanayolengwa kutekelezwa na wadau wote katika ngazi za Halmashauri na Mikoa.
“Maazimio yameshirikisha makundi matatu ambapo kundi la kwanza ni asasi za kiraia,waandishi wa habari vinara na Serikali ambapo maazimio hayo ni; Ujumuishwaji wa programu hii ya MMAM katika bajeti ya mwaka 2024-2025 ambapo OR-Tamisemi itajumuisha programu hii katika bajeti yake,Kufikia halmashauri zote 184 kwani tayari programu hii inatekelezwa katika halmashauri 70 na Uimarishwaji wa uratibu kupitia mwongozo utakaosimamiwa na Maafisa ustawi wa Jamii .
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.