Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WAKUU wa taasisi mbalimbali zinazotoa huduma wilayani Dodoma wametakiwa kuwasilisha makisio ya Mpango na Bajeti zao ofisini kwa mkuu wa wilaya ili mpango wa pamoja uandaliwe kwa ajili ya kuboresha huduma jijini Dodoma.
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akipokuwa akichangia kwenye makisio ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa jiji hilo.
Shekimweri alisema “taasisi mbalimbali wilayani Dodoma kama DUWASA, RUWASA, TANESCO, TTCL ni vema mkawasilisha ofisini kwetu makisio ya mpango na bajeti zetu, ili tukae na kupanga pamoja jinsi ya ku ‘harmonize’ mpango huu mkubwa wa jiji unaochukua karibu asilimai 80 ya mpango wa maendeleo katika wilaya na mipango yenu”.
“Jiji wakisema tunajenga shule Tambukareli, DUWASA nae aone ni muhimu kupeleka maji Tambukareli, TANESCO nae aone ni muhimu kwenye kipaumbele chake kupeleka umeme Tambukareli. Kuliko mradi unakamilika tunaona kama tunafanyiana hisani kwenye kufikisha huduma. Sisi ni serikali moja tunakosea tusipokuwa na mipango inayosomana vizuri” alisisitiza Shekimweri.
Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imekadiria kukusanya na kutumia mapato yenye jumla ya shilingi 128,278,555,369 kutoka vyanzo katika vyanzo vyake vya ndani, serikali kuu, wahisani kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo, utoaji huduma na kujiendesha.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.