Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt. Alphonce Chandika amesema kuwa miongoni mwa Watanzania wenye umri kati ya miaka 15-49 wameambukizwa Virusi vya Homa ya Ini aina ya B, hii ni kutokana na Takwimu za Ofisi ya Taifa wa Takwimu 206-2017.
Dkt. Alphonce Chandika aliyasema hayo wakati maandimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani iliyokuwa na kauli mbiu ya "Wekeza katika mapambano ya Homa ya Ini". Maadhimisho hayo kitaifa yalifanyika Jijini Dodoma katika Hospitali ya Benjamini Mkapa tarehe 28 Julai, 2019.
“kati ya wachangiaji damu 307,835 takribani watu 13,613 sawa na asilimia 4.4 walikuwa na maambukizi ya homa ya ini kwa mujibu wa takwimu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS)” alisema Dkt. Alphonce Chandika.
Dkt. Alphonce Chandika aliendelea kusema kuwa Mwaka 2017, kati ya wachangiaji damu 233,953 takribani watu 11,417 sawa na asilimia 4.9 walikuwa na maambukizi. Aidha, asilimia 0.5 ya wachangiaji damu walikuwa na maambukizi ya homa ya ini aina ya C kwa mwaka 2017 na asilimia 0.3 kwa mwaka 2018.
Vilevile, Dkt. Alphonce Chandika alisisitiza juu ya kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi juu ya athari za ugonjwa wa Homa ya Ini katika jamii na kwa nchi kwa ujumla, huku akisisitiza kuwa Serikali itaokoa kiasi kikubwa cha fedha kinachotumika kwenye matibabu dhidi ya ugonjwa huu wa homa ya ini kama itawekeza nguvu kwenye kinga.
Nae Mkurugenzi msaidizi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba amesema kuwa, huduma hii ya chanjo ya homa ya Ini imeanza kutolewa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa za Sokoture Mwanza, Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi Kilimanjaro, Hospitali ya Rufaa ya Geita, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Hospitali ya Temeke, Hospitali ya Mwananyamala, Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Hospitali ya Muimbili, Moi, Ocean Road na vituo vyote vya mipakani.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika kitaifa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, kushoto ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba, na Kulia ni mwakilishi wa WHO Dr. Christine Chakanyuka Musanhu.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika katika picha ya pamoja na wadau pamoja na Watumishi wa Sekta ya Afya, wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.